Watanzania kweli tuna akili?

Mshana Jr ( @Cage clay ) alimuuliza rafiki yake Kiranga kule nyumbani kama ana akili, Kiranga naye akataka kueleweshwa akili ni nini kabla ya kujibu kama ana akili ama hana akili, mjadala ukaishia hapo. Lakini swali kwamba watanzania tuna akili ama la ni swali linalotakiwa kumtafakarisha kila mtanzania kutokana na aina ya maisha tunayoishi.

Kama tuna akili je tunazitumia ipasavya na itakiwavyo. Hivi malezi ya kwenye familia zetu yanatupa nafasi ya kutumia mbongo zetu kwa kiwango cha kutunza ubinadamu wetu? Kuna tofauti gani kati yetu sisi na Roboti iliyoprogramiwa na kuendeshwa na mtengenezaji wake atakavyo?

Akili ni sawa na nywele kila MTU anazake wengine wana vipala na nywele chache
Hivyo basi watanzania hutofautiana Akili kama nywele zilivyo.

Inategemea na sehemu zilipo

Akili ni nini? Jibu swali hili ili mada yako ieleweke kwa wachangiaji tafadhali!

Ule ubishi wa Mshana na Kiranga ulitosha. Ila kama hujui akilil ni nini basi si lazima uchangie hii mada!

Majibu mepesi juu ya maswali magumu

Inategemeana na akili yako ikoje! Inawezekana unaona swali lako ni gumu na limepewa jibu rahisi, kumbe umepewa jibu gumu lisilolingana na uzito wa swali lako!

Akili tunazo tena nyingi sana…

Tatizo binadamu ni wabishi sana…

Cc: @Mahondaw

Akili zimejaa tele

Nilihisi hichi kitu toka niione ID hiyo ila sikuthibitisha, kwa sasa nishapata jibu

Akili tunazo za kutosha,.tunatofautiana “thinking capacity” tu.

Kumbe na wewe ulivuka mpaka mapema!!

Hahahahaa nilivuka buana kwa neema,.

Kweli kwa neema maana walipofunga walitamani watufunge na sisi tusiwe na akili ya kufanya ukimbizi!!

QUOTE=“Allen Kilewella, post: 1667403, member: 37285”]Kweli kwa neema maana walipofunga walitamani watufunge na sisi tusiwe na akili ya kufanya ukimbizi!!
[/QUOTE]

Hahahahaa ndio maana nikasema watz tuna akili tunatofautiana mauwezo tuu ya ung’amuzi

Kula like rafiki

Nimeipokea rafiki shem darling wangu…

Akili tunazo ila namna tunavyotumia ndo tunatofautiana.

Mimi nisogezee ukoko wa pilau…

Hahah!! Kwanini ukoko mzee wakati pilau lipo