Wadau wa JF mnalionaje wazo la Jamiii Forums kujiunga na Kenyatalk permanently?

Kila mtu duniani hivi sasa anajua namna Dikteta Magufuli alivyoweza kuminya Uhuru wa wananchi wake kujieleza. Akipitisha sheria mbovu za habari kupitia wabunge wake wasiojielewa wa CCM

Kwa hali halisi ya nchi yetu kwa sasa, si vyombo vya televisheni, wala si radio na wala si magazeti yanayoweza kusema yana Uhuru wa kutoa na kupokea habari

Habari peke yake zinazoruhusiwa kutolewa na vyombo hivyo ni habari za kuisifu serikali hii ya awamu ya 5, pamoja na kumpamba Magufuli kwa kila alifanyalo, ndiyo njia pekee ya kusurvive kwa chombo chochote cha habari nchini!

Kwa hiyo siyo ajabu kuona vyombo vya habari kama TBC, Radio Uhuru na Magazeti ya Uhuru na yale yenye mwelekeo wao ya akina Jamvi la Habari na Tanzanite, yakiendelea kudumu katika serikali hii

Lakini vyombo vya habari vinavyoandika ukweli katika lengo tunaloliita constructive criticism, yamejikuta yanafwekwa na TCRA!

Mifano halisi ni magazeti ya Mwanahalisi na Mawio ambayo yamefungiwa maisha

Kwa kifupi hivi sasa Tanzania tumepata mtawala ambaye hataki kukosolewa kwa aina yoyote ile, na chombo cha habari kinachojaribu kufanya hivyo, kinajitafutia dhahama!

Huyu Dikteta Magufuli alipoona amefaulu kuvidhibiti vyombo vyote vya habari vya Umma na vya binafsi nchini, kwa hiyo akaona mitandao ya kijamii ndiyo pekee iliyobaki ambayo inayomnyima usingizi…

Ndipo aliponukuliwa akisema “Angetamani Malaika toka mbinguni washuke duniani na kuizima mitandao ya kiamii” mwisho wa kunukuu

Ndipo hatimaye majuma kama mawili yaliyopita akatimiza azma yake ya kuizima mitandao ya kijamii, ukiwemo mtandao maarufu na unofuatiliwa na mamilioni ya watanzania. mtandao wa Jamii Forum

Angalau wana JF tumepata ahueni baada ya kukaribishwa temporarily huku ukimbizini Kenyatalk

Lakini nimekuwa nikiitafakari sana kauli ya Uongozi wa Jamii Forum inayosema “Asante kwa kuendelea kuwa mvumilivu wakati huduma yetu ikiwa haipatikani. Tutarejea muda mfupi ujao” mwisho wa kunukuu taarifa hiyo ya Uongozi wa JF

Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa, hivi Uongozi wa JF umeshindwa kulipa gharama zinazotakiwa na TCRA?

Jibu hapa ni NO kubwa sana

Sasa tatizio ni nini?

Tatizo la dhahiri ninaloliona hapa ni kuwa jamaa zetu wa TCRA wameongeza condition ya kututaka sisi watumiaji wa JF tudisclose identities zetu!

Hilo jambo haliwezekani kabisa kwa utawala huu wa kidikteta wa Magufuli?

Sasa Mimi napendekeza plan B ambayo Uongozi wa JF uuchukue ni kuongea na Kenyatalk ili wajiunge nao permanently

Hiyo nadhani itakuwa ndiyo the best solution so far under this rule of dictatorship of Magufuli

Mwenyezi Mungu tujalie sisi waja wako watanzania tunaoteseka na utawala huu wa kidikteta wa huyu Magufuli unaominya Uhuru wa kujieleza

Kwa Jamii Forum kujiunga permanently na Kenyatalk, tutakuwa tumepata nguvu ya kumchapa bakora Dikteta huyu Jiwe hadi asalimu amri na kutuachia Urais wetu!

JamiiForums haiwezi kujiunga na kenyatalk permanently, I mean hata kujaribu tu wanaweza wasifanye.

Kinachowezekana ni wanajamiiForums kujiunga na KT, be it partial or permanent.

Wazo zuri. Na huku Kenya talk tunaweza kujiachia tupendavyo. Cha muhimu ni kumwambia ukweli bila kuuma maneno.

mimi hata jamii forum ikirudi kwenye utawala huu nitachangia kwa tahadhari mno, ni bora nibaki huku

Mambo yameshabadilika Ndugu yangu

Sasa hapo haoni watamkamata Melo na Mushi?

Labda watangaze wameiuza ili hata ikiendelea kutumika watakuwa na la kujitetea kwamba hawahusiki nayo

Kwani imejiunga hata temporarily? Hawa ni wakenya wameona fursa tu wakaanzisha section, JF hawahusiani na hawa hata kidogo

Mmhh ntachangia tena baadae

Ngoja tuone…

Cc: @Mahondaw

jamii forums itarudi ila haitakuwa salama tena so cha kufanya ni kuwaomba jamaa hawa wa kenya talk kuanzisha TANZANIAN FORUM hapa pako huru zaidi kulisasambua jiwe na mwanaye bashite

haitasaidia itakuwa ni kukimbia tatizo na kukaa kwny comfort zone, bcz tcra wataweza ht kuizima iyo kt. cha muhim ni jf wakomae tu waangalie namna ya kumaliza hil ikibid ht iyo sheria ibadilishwe

Tumekuwa watoto wa kutangatanga ovyo kisa ni huyu mshikaji
Nalog off

Hapana

Hivi ndivyo ilivyo kwa forum nyingi/zote, hazichagui wanachama, kikubwa tu uweze kumudu lugha inayotumika kwenye forum husika

!
!
Kuna Sheria Inabidi Ziendane Na Miundombinu. Selikali Ya Analojia Haiwezi Kutekeleza Sheria Za Digitali. Wanaumbuka Tu #Mbwakoko

Haiwezekani kwani Watz wengi uwezo wa kufikiri ni mdogo sana.

hata sasa wa kenya wanatuvumilia sana…wataturemove si mda.

Sidhani kama wakenya wanaweza vumilia post za CCM humu… Uchafu na utumbo wa CCM unavumilika Tz tu.

Wazo zuri ila ni ngumu sana kufanikiwa…siioni JF ikirudi hewani,bora tuendelee kubaki hapahapa KT

Hao TCRA mwisho wa mamlaka yao ni Namanga

Hawana uwezo wa kuingia Kenya na kutekeleza sheria zao mbovu, zilizotungwa na wabunge wasiojielewa wa CCM

No JF wafungue registration ugaibuni hasa USA au preferably Europe(western)