Pale kwenye Jamiiforums wabadili pawe Swahili Forums , ila majukwaa wayaache hivyo hivyo.
Naamini watu wengi bado tutaendelea kuwa humu hata JF ikiwa hewani.
Kwanini wasifungue kutokea nchi za nje kama USA, Europe? Why not register there. Mbona ansikia database ya JF iko Ufaransa, sasa kigumu ni nini kufungua Ufaransa?
sure! me nasemea wanaweza kuizuia sis tulio bongo tusiipate bt nchi zingne waipate
Ugenini kuna uhuru kuliko nyumbani
Mbona kama ni hivyo ni simple tu…watu watatumia VPN
Absolutely mkuu
Tangu JF infungwe darasa la Ras Simba lime over flow. Mimi nimekuwa class monitor.
Naona @Babu Asprin bado training haijamkaa vizuri kichwani maana anasua sua hapa sana
Wasio concentrate darasani utawajua tu
Absolutely true
Huyu Jiwe anadhani ana akili zaidi ya teknolojia
Sasa ameona ameifunga JF hapo nyumbani, wanaJF wanajiachia kwa nafasi kutoka nchi jirani!
Huyu Ngosha na wabunge wake wa CCM “weupe” kabisa upstairs…
Hii dunia ya Leo siyo ya kutumia mabavu bila kutumia akili, utaumbuka tuuu
Sasa Magufuli aibu imemkuta
Uzito wa miwani ya Babu napo unampa shida sana
Real talk,dunia ya leo bila kutumia akili ni sawa na bure
Mi nadhani hapa ugenini nini kuzuri tuu.hifadhi hii kama nini ya kudumu mbona poa tuu
Nipo nimetulia tele… tatizo vyuma vimekaza…
Yaani huyu Jiwe anadhani ametukomesha, kumbe ndiyo amejikomoa, kwa kuwa huku ukimbizini ndiyo tunajiachia kwa nafasi kubwa bila bughudha ya kutishwa tishwa
Jibu ni gumu kwani mwenyewe amekiri hapa kuwa ana makoloni mengi. Lakini home kwetu hakuna vyuma.
Ugenini hasa kwa jirani sio permanent solution,kuna wakati serikali za majirani wanatengeneza MOU.
Kama Moi na Nyerere walivyobadirishana wale waliokuwa wakimbizi wa kisiasa kutoka nchi zetu yaani Kenya na Tanzania.Wale wakenya waliporudishwa walinyongwa.
Yaonekana tuna short memory.
Kwa sasa, ninachojua ni kwamba nipo kambi ya wakimbizi nikitafuta hifadhi, basi! Suala la kuwa permanent au temporally litajulikana hapo baadaye kulingana na hali halisi itakavyokuwa…
Lakini tambua kuwa mambo yote haya yanategemea nchi husika ina sheria gani…
Lazima tutambie kuwa Kenya haina sheria za “kijinga” kama za kwetu, kwa hiyo hata hiko unachokiita MoU haiwezi kufanya kazi kwa kuwa hata huyo Kenyatta keshamuona huyo mwenzake Magufuli kuwa “hamnazo” kwa upande wa upstairs