Sijajua Kama Shetani anaweza kugeuka na kuwa malaika ingawa najua upo uwezekano wa Malaika kugeuka kuwa shetani. Nape ni mmojawapo wa watu waliofanya juhudi kubwa sana kwa hila na Ghiliba kuoenesha kwamba uozo ulioko kwenye nchi yetu CCM haihusiki.
Nape na Kinana ndiyo walioleta zile kauli mbiu za “tumetekeleza tunasonga mbele” enzi za Kikwete na kuwaita mawaziri wa Kikwete Mizigo hata kama mbele ya safari waliwapitisha tena kuwa viongozi na wagombea ndani ya chama chao. Lakini ni nani asiyekumbuka tambo na majidai ya Nape aliposema kwamba, kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 CCM LAZIMA ishinde hata ikibidi kwa goli la mkono?
Lakini tangu afukuzwe uwaziri Nape anaonekana kama vile “amebadilika” kwa kuonesha kwamba yupo upande wa wananchi. Kwa mtazamo wangu ni kwamba Nape bado anaendeleza unafiki ule ule wa enzi za Kikwete alipowaita baadhi ya mawazi kuwa ni mizigo. Leo Nape anapoinanga serikali ya chama anachodai yeye atakuwa wa mwisho kutoka, si anatufanyia ghiliba kwamba anapambana na alio pamoja nao wakati anatufanyia sisi maigizo?
Nape sio wa kumuonea huruma acha karma imtafune, baada ya kuhakikisha wamefunga goli la mikono pia alishiriki kuzima bunge na kupitisha sheria ya vyombo vya habari
Huyo Nape ni mnafiki tu kama walivyo viongozi wote wa CCM
Nape hatuwezi kumsamehe kwa kuwa ni yeye aliyelizima Bunge Live kwa kuagizwa na Magufuli wake kwa kisingizio cha gharama!
Yeye Nape alihusika kwa asilimia 100 kuleta sheria hii mbovu sana ya maudhui ya mtandaoni, ambayo imesababisha mtandao wetu pendwa wa JF kuzimwa
Wabunge wa upinzani walijitahidi sana kuipinga sheria hiyo mbovu lakini hatimaye ikapitishwa na wabunge wa CCM kwa kutumia ile kauli ya wengi wape.
Kwa hiyo naunga mkono hoja ya kumweka Nape katika kundi la Mashetani wabaya kabisa ambao nchi hii imewahi kuwapata, licha ya kutaka kujigeuza kinyonga baada ya kutumbuliwa kule kwenye system!
Shetani ni malaika alietaka kumpindua Mungu,sio sahihi au kwa kutoelewa au kwa kukurupuka wapo wanasiasa wanafikiri shetani si malaika.
Nape tumsamehe alikuwa hajui hatendalo.
Wengi wanapopata nafasi ya kutumikia wananchi mara zote huwa wanajisahau na kujipa matumaini kuwa watadumu siku zote…kimbembe huja baada ya kutoswa na system inayoongoza hapo ndipo akili huwarudia na kujuta.
Nape yule aliyetoka hadharani kutetea hizi sheria mbovu na kuzima bunge live , Yule ndio Nape halisi kabisa.
Maana wanasema kadri Nyani anavyozidi kupanda juu ndio sehemu ya nyuma inavyozidi kuonekana kwa uzuri, hivyo yule ndio alikuwa Nape halisi.
Ila huyu wasasa anayeshinda Twitter na post zake za mafumbo ili aonekane mtakatifu na hana hatia, huyu ni Nape Fake na ni wa kumuogopa.
Amini nawaambieni ikitokea “jiwe” likamteua kwa mara ya pili jamaa atakubali uteuzi huo na kurudi kwenye uhalisia wake.
Msiwaamini sana Maccm ya aina hii ya Nape, huyu bado ni Shetani tu.
Mimi sitamlaumu mtu yoyote kwa kuwa CCM au Upinzani sababu vyote ni vyama vya siasa na ndivyo demokrasia ilivyo
Ila SITAKUSAMEHE kwa kuhubiri chuki na ukabila kwa watanzania ili ufaidike tu kisiasa
Nape Nnauye alikua akichonganisha watanzania kikabila ili wachukie upinzani, ni siasa za kipumbavu sana hizi kwa kiongozi wa chama kitaifa kuzifanya na hatakiwi kuaminiwa hata kidogo kwa lolote