Namna ya kuagiza bidhaa mtandaoni (Online) eBay, Amazon

Habari naomba kufahamu namna ya kuagiza bidhaa mtandaoni, kutoka katika masoko ya eBay, Amazon na BestBuy.

Kwa maana nimejaribu kuwatumia ma Agent hawa EasybuyAfrica naona wananizingua tu, kila nikiagiza mzigo wanadai seller ni scammer nimeagiza zaidi ya mara nne ila hakuna nilichoambulia,.
kwa hiyo naomba kujua nitaagizaje na mzigo unifikie Tanzania, napatikana mikoani.

Mwl, RCT, MziziMkavu

Wanakuja mkuu

Alikuwa anatoa sana namba yake kule JF kama unayo mwambia aje huku ili aje aandike uzi wake kama ule maana wengi sana walisaidiwa kupitia uzi ule.

Sawa nawasubiri, kwa maana kuna baadhi ya bidhaa nazihitaji

Aisee ile JF ORIGINAL imekamatwa na kila kitu

Mambo mengi sana yamepotea mkuu, hadi kuja kuyarejesha itachukua muda sana

Ila huku KE hata wenyeji watatusaidia kwa maana hakuna namna

Kumekuchaaaaaa

Ukitaka kurahisisha mambo kuwa ni vitu vifuatavyo;

 1. Sanduku la Posta (sio lazima ila ni vizuri na muhimu kuwa nalo)

 2. Debit card hapa chukua equity, utafungua ndani ya siku moja kama una moja ya ID zifuatazo, kadi ya mpiga kura, kitambulisho cha utaifa au leseni ya udereva. (Nimechagua equity kwasababu hawana mlolongo kufungua account ukiwa tu na moja ya hizo ID na 10000, utapata card yako yenye vigezo vyote vya kufanya manunuzi mtandaoni.

 3. Kufungua account ktk mitandao unayotaka kufanya manunuzi, Unaanza paypal, ebay, aliexpress, banggood nk.

 4. Paypal ni muhimu kwasababu itasimama katikati kati ya muuzaji na mnunuaji na pia itahusika kuchota pesa kutoka kwa account yako ya bank na kumlipa muuzaji, na ikitokea kuna tatizo lolote kuhusu bidhaa watahusika kurejesha pesa zako, endapo hujapokea bidhaa yako, au kama imekuja tofauti na ulichonunua. Ukishajiunga paypal unatakiwa ku link card yako ya bank kwa paypal kwa ajili ya kukamilisha miamala ya manunuzi, taratibu za kulink ni rahisi, ukishapata card yako kuna taarifa unapaswa kujaza paypal kama card number na exp date, na security code ya card yako, kisha utakatwa kiasi cha kama $2.x, ukienda kwenye bank statement utaona details za huo muamala zitakua na pincode kwa ajili ya kufanya verification ya card yako kwenye mtandao wa paypal, ukimaliza hapo card yako ipo tayar kufanya miamala.
  Ntaongezea mengine …

kwa ufupi sana,

napendelea aliexpress/alibaba zaidi ya ebay

1.uwe na sanduku la posta (slp)
2. kadi ya visa/masta (yenye mkwanja)
3. nenda bank husika, waambie waiwezeshe kadi yako ifanye ‘online purchase’…hapa ushamaliza

a. ingia aliexpress.com/
b. search bidhaa uitakayo
c. cheki feedbacks za previous buyers wa iyo bidhaa ili seller asiwe ‘scammer’

d. akiwa poa, chagua shipping utakayoiweza ( hua napendelea aliexpress standard shipping , usd 13/item, 2 weeks kufika ) , cheki total price = item + shipping price

e. click ’ buy now ’ , itakuja page mpya utajaza details zikiwemo SLP , namba ya sim, visa card details

f. watakata kiwango/mkwanja husika kutoka katika kadi yako then apo utakua umemaliza.

g. mzigo utachukua siku kadhaa mpaka kufika, utapigiwa sim na watu wa posta ukauchukue!

AYO NI MAELEZO KWA UFUPI

Mimi nimewahi kununua mara 2 kupitia Ebay, hatua za kufuata ni hizi

 1. Inabidi uwe na Credit/Debit card, mimi nilitumia ya CRDB ila ina mlolongo kidogo maana CRDB huwa wanakutaka ujaze form ya kuomba huduma ya Online Purchase ndipo kadi yako iweze kufanya manunuzi, NBC wao kadi zao zinakuwa active mara baada ya kupewa unaweza kufanyia manunuzi.
 2. Ukishakuwa na kadi, fungua account ya paypal, ni muhimu kwa usalama wa pesa zako ukisha fungua weka taarifa ya kadi yako kwenye account ya paypal hakikisha bank una pesa kidogo kama 10 elfu hivi, account ikiwa empty watakataa.
 3. Ingia Ebay na tengeneza account na uweke taarifa za ukweli ikiwa ni pamoja na anwani yako ambayo utapenda mizigo ikufikie.
 4. Kuna baadhi ya bidhaa huwa muuzaji anaweka wazi kuwa hasafirishi kuja Tanzania hizi zina njia tofauti kuzipata, mimi nitaelezea zile zinazoweza kufika Bongo.
 5. Chagua bidhaa uitakayo (hakikisha muuzaji ni Top Rated Seller) hii ni kwa usalama wa fedha pia
 6. Chagua Buy it Now
 7. Chagua kulipa kwa paypal, ingiza email na pasw ya paypal account yako, hapo utaona taarifa za kadi yako zimekuja automatically(kumbuka ulizijaza kule kwenye paypal account)
 8. Thibitisha anwani ya kutumiwa mzigo na fanya malipo.

Mimi nilisubiri bidhaa kwa siku kama 15 ikanifikia toka US na niliyoagiza toka china ilichelewa kidogo maana zilitumwa kwa posta kawaida.

Ahsante sana kwa mchanganuo mzuri aisee nakupa Kongole

Nakutakia Eid Mubarak

Ahsante sana kwa maelekezo mazuri nashukuru sana

Kila la keri, pia kama kuna shaka Ebay watakushauri u council muamala na watakurudishia pesa yako muda huo huo, kimsingi kwakupitia Ebay sijawahi kupoteza hata shilingi mia

Umeshajaribu Kikuu?wako vizuri sana nimewatumia several times sijajutia…

daaaah

Kikuu sija wahi kutumia, sema jana nimiangalia wana bidhaa chache mno haswa za ki electronic

Uko sahihi,ila wamejipanga vizuri sana sijajua tu wanajitihada gani wanafanya kujitangaza ili waweze kuwa na status kubwa kama wenzao wengine…

mkuu kwa uzoefu wako ukiachilia CRDB na NBC ni bank gani zingine ambazo hazina mlolongo katika kusajili card kwa online purchase?

Bank ABC