Mvumbuzi wa kipimo cha DNA apongezwe? Amevunja ndoa nyingi.

Mradi hufahamu kuwa huyu ni baba yako na anakupenda maisha yanaendelea. Sasa huyu mvumbuzi wa kipimo amezua tafrani kwenye jamii.
Kweli huyu anastahili pongezi hasa kutoka kwetu wakina mama?

Ila wakina mama wana siri…wanajua kabisa mtoto sio wa baba…alafu kimya…

Mungu anawaona

Tukiweka kwenye mizania ya haki kuna upande utampongeza na kuna upande utamlaumu

Napenda kuwaona akina mama wakitumia hekima na upendo. Pia napenda kuwaona wakiwasitiri waume zao kwa kuhakikisha wanawapa watoto ambao ni wao hata kama wanamichepuko. Hivi ni kweli siku zako za hatari huzijui hata ushike mimba ya mchepuko na kumzawadia mumeo?. Binafsi nimeoa. Nimemuoa ambaye alikuwa mpenzi wangu tukiwa shule ya msingi. Mimi mbele yeye nyuma yangu. Nimembikiri mwenyewe. Ni mwanamke wa kwanza kwenye maisha yangu. Nami wa kwanza kwake. Katika harakati za masomo tulipotezana kwa muda. Hatimaye yeye akazaa. Baadaye tukakutana na mwishowe kuoana. Amenizalia watoto wawili. Wa kike na kiume. Kumbuka yeye anao watatu. Siku zote namsisitiza na analijua hilo. NIKO TAYARI KUMUOA MWANAMKE MWENYE WATOTO HATA WATANO, ILA SIO KUISHI NA ALIYENILETEA MIMBA KWENYE NDOA YANGU. Sipendi hata kusikia. Baba yangu mzazi amezawadiwa mmoja na mama mdogo. Yaani mke wake wa sasa. Mjomba ake na mke wangu, amezawadiwa wawili na mkewe ambaye wameachana. Kila anayewaona wale watoto anajua dhahiri kuwa ni wa nani. Mama mkwe wangu ameachika, amemzawadia mumeo mtoto mmoja aliyepelekea ndoa kuvunjika. Huyo mzee sio baba yake mke wangu. Kwa kifupi mama mkwe wangu amezaa na wanaume zaidi ya wanne. INAUMIZA SAANA. Kijijini kila kitu huwa hadharani. EE MWENYEZI MUNGU NINUSURU NA JANGA HILI. WANAUME TUNAUMIZANA SAANA KUPITIA WANAWAKE. MKE WA MTU UNAMTIA MIMBA???

Yanini kujipa presha na baadaye ufe mapema kwa stress? Kama umeamua kulea usianze kuhojihoji kama mtoto ni wako, na ikifikia hapo ni bora uanze kujihoji kwanza wewe, je, ‘mshua’ kweli ndiye baba yako?..

ivi icho kipimo hakijawahi kuongopa

Binadamu ndio huongopa, anaweza kukupa majibu tofauti na yaliyopo kwenye kipimo. Utajuaje?..

Wanawake wana siri nyingi sana wanaume tuwe makini kwenye kuchunguza watoto .Jamaa yangu kazaa na mke wa mtu halafu jamaa hajui ,huko Facebook mapicha tu ooh my first born!!!

wanaume tuna mtihani mkubwa saana juu ya wake zetu.mbaya zaidi sisi wenyewe ndio twaumizana.

Hizi ni stress yaani unalea mtoto unamsomesha wmekuwa kwenye miaka kumi na kitu unaambiwa sio wako utakufa mapema

Hivi mwanamke mpaka inafikia hatua hiyo ya kumdanganya mwenzio kuwa hawa watoto wote wako kumbe sio hivi unamtakia mema?

Kuna Mnaija alipata kiharusi baada ya kugundua watoto wote wanne sio wake.

Umeongea kwa uchungu sana

Kaleta ukweli penye uongo…

Cc: @Mahondaw

Unajua wazee wetu wanasema siku hizi maadili hasa kwenye ndoa yameharibika, mambo ya kutoka nje ya ndoa yamekua mengi na watoto wa nje ya ndoa wanazaliwa ndani ya ndoa na kuumbuliwa na kipimo cha DNA. Lakini kiukweli hata enzi hizo mambo ya kuchapiana yalikuawepo sana tu na watu wamelea sana watoto wasiokua wao kibaiyolojia, sema hapakua na vipimo kama hivi vya DNA kwa hivyo maisha yakaendelea tu

Wanawake walibakwa wakiwa wanatafuta kumi, kwenda kuchota maji au shambani peek yao. Ilikuwa ni aibu kusema kuwa ukibakwa kwa mwanamke. Pia haya mambo ya hali ya uchumi, mama alipata buzzy na kuokoa hali ya nyumbani pasi kumdharau mume wake. HIV ndiyo iliondoa ndoa nyingi kwa style hii miaka ya 90’s

Inamaana enzi hizo kuvumiliana kulikua kukubwa au jamii ilikua gizani? Ukiangali hata unyanyasanyi wa kijinsia kwa watoto unaofanywa na ndugu wa karibu ulikuwepo lakini mambo yalifunikwa na kuonekana ni kinyume na maadili kuyatoa hadharani

Jamii ilikuwa gizani sana na bado iko gizani

Zamani ukiolewa mwaka umepita hakuna majibu bibi na mashangazi wanakuita wanakutafutia wa kukupa mimba ili umstiri mumeo

We still have a long way to go Sky, hebu angalia katika nchi zetu za Afrika kujenga matundu ya vyoo kwa wanafunzi au kufungua jengo la maabara ya kufundishia katika shule ya sekondari ya kata ni tukio linalofanywa na kiongozi wa kitaifa na yaweza kua habari inayokuchukua umuhimu wa kwanza katika habari za kitaifa kwenye vyombo vyetu vya habari! Hii ni karne ya 21 lakini tunaishi maisha ambayo wenzetu waliishi karne ya 17 nadhani

Hilo usemalo ni kweli kabisa Sky, wanawake wamepitia magumu sana kwa jina la kulinda heshima