Gumzo la Taifa: Diamond aibukia kwenye show ya Davido iliyoandaliwa na Cloud Media

Katika hali isiyotegemewa msanii maarufu Duniani na Afrika nzima Diamond Platnumz ametoa sapraizi ya aina yake baada ya kuibuka kwenye show iliyoandaliwa na Clouds Media na kushea stage moja na mkali kutoka Nigeria Davido,wasanii hao wawili waliimba wimbo wao wa Number one remix huku wakikonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye ukumbi wa Next door Arena Masaki jijini Dar.

Kabla ya kufika mahali hapo pia Diamond alitoa sapraizi nyingine kwenye usiku wa Kusi,show iliyofanyika Dar Live Mbagala na kuimba kwa pamoja na msanii anayetamba kwa sasa kutoka WCB harmonize ambapo waliperfom vibao kama Ngoja na Kwangwaru.

Mpaka nawaletea habari hii gumzo limebaki huko mitandaoni na mijadala mikali kwamba huenda huu ndio ukawa mwanzo wa tamati ya mgogoro uliopo kati ya WCB na Clouds Media huku mashabiki wengine wakisema huenda Clouds chini ya Kusaga wameamua kumuita Diamond kumuonyesha wao hawana tatizo naye isipokuwa bwana Ruge ambaye anaumwa hoi bin taaban na hayuko bongo mwezi mzima sasa ndiye mwenye chuki zake binafsi.

Toa Maoni Yako.
Habari na @chinga one wa JF kwa sasa mkimbizi nchini Kenya Count ya Madhare ndani ya Kenya Talk.
[ATTACH=full]176701[/ATTACH][ATTACH=full]176702[/ATTACH]

Always ruge wins

He is sick anapumulia mashine figo zimefeli yuko India,wenzake wamemgeuka…

Whatever all in all mshindi ni ruge awe duniani au ICU jamaa bado ni mmiliki wa clouds

Inabidi wakati mwingine ndugu wakigombana,tusiingilie

Shika jembe ukalime

What if wao CMG ndo wamemdondokea D?

Halafu pia hii show haikuandaliwa na Clouds,walipewa kazi tu ya kupromote

Wcb walivyo na sifa wangeshatangaza zamaan

Na je km Davido ndio kamuta D?

hhahahaha. Ruge must have turned in his death bed.

Mkuu inaonekana inakuuma sana kusemekana dai ka bow down kwa ruge ee?

Duh Ruge ni nomaaaa

Alieiweza hii vita ni komando Jide tu

Hawa wote ni watoto wa baba mmoja,ata wakogombana siku watakutana kwenye kikao cha familia

Mambo yao waachieni wenyewe…

Cc: @Mahondaw

Sema diamond kwel anapendwa mana ukumbi uliwaka kwa shangwe alivyoingia

[ATTACH=full]176876[/ATTACH]

Wewe comments zako tu zinaonyesha ni certified hater wa Diamond.

Hahahahahahahaha aiseee

ila naona kama Diamond ndiyo mshindi. Yuko behind enemy line anafanya yake. ogopa sana " Mutu ya hivyo"