Habari ma-Villagers/Strangers! Pole sana kwa ukimbizi. Binafsi baada ya malaika wa kuifunga Jf kushuka na kufanikisha zoezi nimeamua nitie maguu kabisa huku kwa majirani… kwa sasa naishi maeneo ya Kawangwale nje kidogo ya Nairobi.
Sasa twende kwenye mada, baada ya kufikiri kwa kina na kutafakari kwa kina nimepata jibu kwamba wanawake ni viumbe watata mno japo ni dhaifu kwa misuli.
Ni hivi… utakuta mwanamkke kaolewa lakini anamlalamikia mama mkwe kuwa anaingilia ndoa yake hivyo kumnyima uhuru wa kujinafasi ndani ya ndoaye. Oooh mamamkwe anasema nina kiburi, sina heshima na mambo mengine kedekede.
Lakini cha kushangaza huyu huyu anayelalamika akizaa watoto nao wakaoa anafanya yale yale aliyokuwa analalamika kufanyiwa na mkwewe, tulitegemea kwakuwa aliyaona ni mabaya basi yeye asingeyafanya.
Kuna mawifi wanaoingilia ndoa za kaka zao na kutaka kufanya maamuzi kana kwamba ndoa ni zao, kutaka kumpangia wifi yao nini cha kufanya, lakini wao nao wakifanyiwa hivyo na wifi zao (dada wa waume wao) wanaanza kulalamika , oooh mawifi wanaingilia ndoa zetu… wanasahau kuwa nao wanaingilia ndoa za mawifi zao.
Kuna wanawake waliwahi kuwa Ma house girl wakafanyishwa kazi kama watumwa na manyanyaso mengi na pengine kudhurumiwa malipo yao. Mungu si Abdalla nao maisha yakaja kuwanyookea nao wakawa na wasaidizi wa kike nyumbani, tulitegemea wawe watu wenye huruma kwa hawa wasaidizi wao, lakini baadhi yao wamekuwa wakatili mara dufu kwa kuwatendea mabaya ya kila namna.
Mpaka hapo nikagundua kuwa akili za wanawake anazijua muumba wao.