Katika sakata la korosho linaloendelea, Mwanasheria Mkuu wa serikali, Dr Adelardus Kilangi, ametuhumiwa kulipotosha Bunge hilo kwa kusema uongo kuwa wao serikali wanatekeleza amri ya mahalama katika hukumu iliyotolewa miaka ya nyuma kuwa ilibatilisha sheria iliyokuwa ikitoa kwa bodi za korosho mapato yanayotokana na (export levy) ya asilimia 65, ambapo asilimia 35 inayobaki 35 ilikuwa inabaki kwenye mfuko Mkuu wa serikali ambayo ni Hazina
Mwanasheria huyo amejipalia “makaa” kwa kutoa kauli hiyo ya uongo bungeni baada ya wabunge kuja juu kuwa kauli yake sio ya kweli kwa kuwa hakuna hukumu ya aina hiyo ambayo imewahi kutolewa na mahakama yoyote hapa nchini
Kwa hiyo wabunge wakatoa pendekezo kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kuiagiza Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge iitishe kikao chake Mara moja ili kumjadili Mwanasheria huyo Mkuu wa serikali na kumwajibisha, kwa kulidanganya Bunge
Mkuu umepiga mulemule. Awamu iliyopita serekali ilikuwa inalionea bunge aibu ikawa inatii baadhi ya mambo. Ila awamu hii imeligeuza hilo bunge kama bunduki isiyo na risasi. Ndio maana ni rahisi waziri nk, kuongea uongo wa wazi bungeni bila kuchukuliwa hatua. Kibaya zaidi matumizi yaliyoidhinishw nje ya bunge yameshika kasi na hakuna kitu bunge linafanya.
Tatizo la nchi hi ni kwa kuwa hatuna uchaguzi ulio wa Uhuru na haki…
Kama kweli nchi ingekuwa inaendesha chaguzi huru na haki, Magu asingepata kiburi cha kuendesha nchi kama ambayo anaendesha familia yake…
Kiburi chote anakuwa nacho kwa kuwa ana Tume yake ya uchaguzi na Jeshi lake la Polisi ambalo anajua akiliagiza lizime protests zozote, akiwa kama Commander In Chief litatii…
Lakini anachosahau Magu ni kuwa katika historia ya dunia hii, haajawahi kutokea toka Dunia inaumbwa kwa utawala wowote kuishinda nguvu ya Umma
[FONT=tahoma]Watendaji wamekuwa waoga mpka wanashindwa kutumia weledi katika nafasi zao hii inatokana na mtu kufanya kazi kama jeshi la mtu mmoja badala ya taasisi hatari kubwa mbeleni mengi yatakwama kutokana na kumuogopa kiongozi mkubwa na wanashindwa kumwambia ukweli.[/FONT]
Mkuu kama Spika anafikia hatua anatumika kulitishia bunge lake kuwa wasipokubalina na serikali basi bunge litavunjwa…na wengine hawatarudi bungeni hapo ujue wazi hatuna bunge zaidi ya kikundi cha wachache wanaojali matumbo yao.