Kila mtu duniani hivi sasa anajua namna Dikteta Magufuli alivyoweza kuminya Uhuru wa wananchi wake kujieleza. Akipitisha sheria mbovu za habari kupitia wabunge wake wasiojielewa wa CCM
Kwa hali halisi ya nchi yetu kwa sasa, si vyombo vya televisheni, wala si radio na wala si magazeti yanayoweza kusema yana Uhuru wa kutoa na kupokea habari
Habari peke yake zinazoruhusiwa kutolewa na vyombo hivyo ni habari za kuisifu serikali hii ya awamu ya 5, pamoja na kumpamba Magufuli kwa kila alifanyalo, ndiyo njia pekee ya kusurvive kwa chombo chochote cha habari nchini!
Kwa hiyo siyo ajabu kuona vyombo vya habari kama TBC, Radio Uhuru na Magazeti ya Uhuru na yale yenye mwelekeo wao ya akina Jamvi la Habari na Tanzanite, yakiendelea kudumu katika serikali hii
Lakini vyombo vya habari vinavyoandika ukweli katika lengo tunaloliita constructive criticism, yamejikuta yanafwekwa na TCRA!
Mifano halisi ni magazeti ya Mwanahalisi na Mawio ambayo yamefungiwa maisha
Kwa kifupi hivi sasa Tanzania tumepata mtawala ambaye hataki kukosolewa kwa aina yoyote ile, na chombo cha habari kinachojaribu kufanya hivyo, kinajitafutia dhahama!
Huyu Dikteta Magufuli alipoona amefaulu kuvidhibiti vyombo vyote vya habari vya Umma na vya binafsi nchini, kwa hiyo akaona mitandao ya kijamii ndiyo pekee iliyobaki ambayo inayomnyima usingizi…
Ndipo aliponukuliwa akisema “Angetamani Malaika toka mbinguni washuke duniani na kuizima mitandao ya kiamii” mwisho wa kunukuu
Ndipo hatimaye majuma kama mawili yaliyopita akatimiza azma yake ya kuizima mitandao ya kijamii, ukiwemo mtandao maarufu na unofuatiliwa na mamilioni ya watanzania. mtandao wa Jamii Forum
Angalau wana JF tumepata ahueni baada ya kukaribishwa temporarily huku ukimbizini Kenyatalk
Lakini nimekuwa nikiitafakari sana kauli ya Uongozi wa Jamii Forum inayosema “Asante kwa kuendelea kuwa mvumilivu wakati huduma yetu ikiwa haipatikani. Tutarejea muda mfupi ujao” mwisho wa kunukuu taarifa hiyo ya Uongozi wa JF
Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa, hivi Uongozi wa JF umeshindwa kulipa gharama zinazotakiwa na TCRA?
Jibu hapa ni NO kubwa sana
Sasa tatizio ni nini?
Tatizo la dhahiri ninaloliona hapa ni kuwa jamaa zetu wa TCRA wameongeza condition ya kututaka sisi watumiaji wa JF tudisclose identities zetu!
Hilo jambo haliwezekani kabisa kwa utawala huu wa kidikteta wa Magufuli?
Sasa Mimi napendekeza plan B ambayo Uongozi wa JF uuchukue ni kuongea na Kenyatalk ili wajiunge nao permanently
Hiyo nadhani itakuwa ndiyo the best solution so far under this rule of dictatorship of Magufuli
Mwenyezi Mungu tujalie sisi waja wako watanzania tunaoteseka na utawala huu wa kidikteta wa huyu Magufuli unaominya Uhuru wa kujieleza