Wezi wa rambi rambi wako mkao wa kula tena

Yalipotokea maafa ya tetemeko Kagera wananchi na taasisi mbali mbali walitoa michango ya pesa na vitu ili kuwasaidia waathirika wa tetemeko lile. Katika hali isiyokuwa ya kawaida mkuu wan chi alipokwenda kule baada ya muda mrefu kupita akasema michango itaelekezwa kwenye kurekebisha miongo mbinu kinyume kabisa na lengo la michango na wachangaji. Kana kwamba hiyo haikutosha akatoa maneno ya kuumiza zaidi kwa kuhoji kuwa kwani ni yeye ndiye aliyeleta tetemeko. Akaendelea kusema mkoa ule umekuwa na mabalaa yote vita, ukimwi, mto ngono na katerero ni huko huko. Badala ya faraja kutoka kwa chief comforter au mfariji mkuu, wakaambulia masimango na kejeli huku rambi rambi na misaada ikichukuliwa na serikali. Viongozi wa upinzani waliowahi kwenda kufariji na kutoa misaada kule wakashambuliwa kuwa wanageuza maafa kama kete ya kisiasa na wengine hadi kuzuiwa kutoa misaada. Watanzania ni wapole sana kama kawaida yao wakamwachia Mungu.

Haukupita muda mrefu sana ikatokea ajali kubwa iliyoua wanafunzi 32 wa shule ya Lucky Vicent huko arusha. Kama kawaida watanzania ni wema na watu wa kujitolea. Wakachanga rambi rambi kwaajili ya wafiwa. Katika hali ya kushangaza serikali mkoani humo ikatangaza kuwa baadhi ya pesa za rambi rambi zitatukika kukarabati hospitali ya Mount Meru. Hili likawa kosa la pili tena kufanywa na serikali kutokana na maafa. Kana kwamba hiyo haitoshi hata viongozi wa dini na wa vyama vya upinzani walioamua kwenda kuhani wafiwa shuleni moja kwa moja walikamatwa.

Matukio haya mawili yalipunguza sana imani ya wananchi kwa serikali inapotokea kuna maafa. Imani ya wananchi ilipotea kabisa kutokana na kauli na matendo ya viongozi wa serikali.

Hivi sasa tupo kwenye maombolezo ya vifo zaidi ya 220 vilivyotokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere. Lakini hata kabla zoezi la uokoaji na upoaji kukamilika serikali imekwenda kufungua akaunti ya rambi rambi. Hili limewashangaza wengi. Kwanza kufungua tu akaunti ni dalili ya serikali kukubali kutokuaminika tena kwenye michango ya majanga. Lakini hata hivyo kulikuwa na uharaka gani?! Je serikali haina pesa za kugharimia tatizo hilo mpaka ikusanye rambi rambi katikati ya uokoaji na uopoaji? Mbona inatumia mabilioni kwaajili ya chaguzi za marudio za viongozi wanaojiuzulu ambazo hazina tija kwa wananchi wanyonge wa nchi hii? Wananchi mbali mbali ukifuatilia maoni yao hawana hamu tena na usimamizi wa serikali katika michango ya majanga kama haya ambapo wengi wanaapa kutotoa ikibidi watawapa wafiwa wenyewe moja kwa moja

Pamoja na kasoro hiyo mwanzoni baada ya kufungua akaunti alikaririwa waziri Jenister Mhagama akisema michango katika akaunti hiyo itakuwa ni kwaajili ya wafiwa na familia za marehemu tu. Hiyo ilianza kidogo kurudisha imani ya wananchi. Lakini tamko la serikali kupitia kwa waziri mkuu jana wakati wa mazishi kuwa sehemu ya rambi rambi hizo itatumika kujenga uzio katika makaburi ya watakaozikwa eneo moja na mnara wa kumbu kumbu limekuwa la kuchanganya zaidi kwa wananchi wengi. Kwamba inakuwaje tena serikali inapanga matumizi ya pesa za rambi rambi ambazo watu na taasisi wanatoa kwaajili ya waathirika na siyo zake? Kama serikali inaweza kutumia mabilioni kwaajili ya kurudia chaguzi za wabunge na madiwani wanaojiulu kwa hiyari yao na kujenga ukuta wa zaidi ya kilometa 22 katika mgodi wa madini wa Mererani inashindwaje kujenga uzio usidi nusu kilometa na mnara wa kumbu kumbu? Je wale ambao ndugu zao hawakuzikwa hapo ukuta huo iunawasaidia nini? Kwakweli hicho kipengele waziri mkuu kama angeshauriwa vizuri asingekisoma kabisa kwakuwa kinatengua maelezo aliyotoa waziri husika na kuwazindua wananchi kuwa yale yale ya Kagera na Arusha yanakuja Mwanza.

Kama nilivyosema awali wananchi wengi hawana imani tena na ushiriki wa serikali katika kukusanya michango ya maafa hata wanaojitokeza sasa utakuta ni mashirika au makampuni ya kibiashara ambayo katika fani ya biashara hiyo nayo ni njia moja wapo ya kujitangaza ingawa kama si mtu wa biashara hutaelewa kabisa. Wengine ni mashirika ya hiyari kama Lions na Lotary nk. Lakini watu binafsi sasa wamejengewa utamaduni mpya kabisa ambao hatukuwa nao awali wa kutoiamnini serikali katika makusanyo ya majanga.

Ushauri wangu kwa serikali ni kuwa serikali inapaswa kurudi nyuma na kuangalia ilipojikwaa kwani hii siyo dalili nzuri kwa serikali kutoaminika na wananchi wake kutokana na mifano niliyotaja hapo juu. Serikali iachie shughuli kama hizi kwa vikundi vya kijamii na mashirika ya hiyari kukusanya na kutawanya misaada ila yenyewe itoe kile kilicho chake na kikipangia inavyotaka kwani inapaswa kujua michango ya rambi rambi na maafa ni kwaajili ya kufariji na kusaidia waathirika siyo misaada ya maendeleo au kodi ambazo serikali inaweza kuingilia na kuipangia shughuli nyingine. Kuna mambo serikali inafanya mpaka unajiuliza hivi mshauri wa serikali ni nani? Mbona spika katuambia kwenye chama cha CCM, wabunge wa CCM na serikali kumejaa watu wenye masters, madokta na maprofesa ukiacha wenye first degree? Kama hivyo ndivyo wanavyoshauri wenye degree, masters, Phd na profesaz basi ni bora wawapishe wasio kuwa na elimu hizo kwani inaonekana wazi kuwa watu wanaweza wakasoma sana lakini wakawa hawajaelimika ila wanajigamba kwa kujitambulisha kwa kuanza majina yao na Dk. Prof, Injinia au mhandisi nk!

https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/388/388909.jpg?1474628375

Hawa jamaaa sio kabisaaaaa

Na kale kaandunje ka bongo mavi hakajatia guu huko maana kwa kupiga rambi rambi kako vizuri.

Awamu hiii wamenoa aiseee

Wanalaani sana,raia walivyoanza kukumbushia ya kagera na arusha.

Mbonà wmeshakula rambi rambi robo. I promise you yote itaisha

Hili jamaa ni jizi la kutupa halina woga wala halina aibu.

Haaaaahaaaaaa

Steve Nyenyere weka mbali na rambi rambi

Heri ya Stephen nyerere