Nafurahishwa na juhudi za hawa vijana wetu katika kazi yao ya muziki na namna wanavyoupigania kuhakikisha unafikia hatua fulani. Pia uwekezaji walioufanya (TV na Redio) ambavyo vinaonyesha mwanga wa kuleta ushindani katika soko la burudani ambapo ushindani huo unaweza kuwaletea neema wasanii, according to Diamond (CEO) amesema mwakahuu wataandaa show inayoitwa WASAFI FESTIVAL na kuhakikisha wanawabana wadhamini watoe pesa ya kutosha ili wasanii walipwe pesa nzuri. Kwangu mimi hii kama itatekelezwa itakuwa ni hatua nzuri kwenye ‘kiwanda’ hiki cha muziki, italeta ushindani hata kwa kwa waandàaji wengine wa matamasha (i.e CMG) watalazimika kuwalipa wasanii vizuri ili kuendana na wenzao na hivyo kuleta neema kwa wasanii kufaidi jasho lao. Thread hii ni maalumu kwa ajili ya kuleta updates ya WASAFI TV/RADIO, WASAFI FESTIVAL,shows, nyimbo mpya, na habari nyingine zinazohusu muziki wao…
Video: Press conference ya WCB na waandishi wa habari ikizungumzia uwepo wao rasmi kwenye king’amuzi cha Startimes ambao Diamond na management yake walizungumza pia kuhusu Wasafi Festival na mambo mengine mengi https://www.youtube.com/watch?v=I9r5wBeX3Z8
Diamond Platnumz alivyo’surprise’ kwenye show ya Davido Club Next Door Arena siku ya IDD pili na kulipua shangwe la kutosha. Tukio hilo lilizua gumzo mitandaoni ukizingatia moja wahusika wa maandalizi ya show hiyo ni Clouds Entertainment ambao siku za hivi karibuni wameonekana kuwa na ‘beef’. https://www.youtube.com/watch?v=G-cb1RMJ3bs
Harmonize ‘Kondeboy’ kwa kushirikiana na Darlive waliandaa show kubwa na kuhudhuriwa na mashabiki wa kutosha, moja ya tukio ambalo bado linatrend U-Tube na kuzua gumzo mtandaoni ni kitendo cha Diamond Platnumz kuvamia jukwaa wakati Kondeboy anaperform na kuibua shangwe kubwa iliyopelekea Harmonize kushindwa kujizua na kutokwa na machozi ya furaha…
Kwenye sherehe za IDD karibu wasanii wote wa WCB walikuwa bize, baada ya Rayvanny kupokelewa vizuri Igunga, akahamishia mashambulizi Tanga na show nilikuwa kama hivi… https://www.youtube.com/watch?v=viGAj2BphM4