Friday, October 5, 2018
[SIZE=7]Wanafunzi 17 wadaiwa kulawitiwa Kilimanjaro[/SIZE]
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/4793492/highRes/2132249/-/maxw/600/-/q3ywl0z/-/ulawiti+pic.jpg
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah.
[SIZE=5]Kwa ufupi[/SIZE]
[ul]
[li]Aliyefichua unyama huo ni mmoja wa wanafunzi hao ambaye baada ya kubakwa alitupwa kichakani na kupatikana siku tatu baadaye na kueleza kuwa alifanyiwa kitendo hicho na wenzake 16[/li][/ul]
By Fina Lyimo na Bahati Chume, [email protected]
Hai. Wanafunzi 17 wa shule za sekondari wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamekiri kulawitiwa, huku baadhi ya wazazi wakisema walifanyiwa kitendo hicho Septemba 28, siku ya mkesha wa mwenge.
Aliyefichua unyama huo ni mmoja wa wanafunzi hao ambaye baada ya kubakwa alitupwa kichakani na kupatikana siku tatu baadaye na kueleza kuwa alifanyiwa kitendo hicho yeye na wenzake 16.
Alipoulizwa na MCL Digital leo Ijumaa Oktoba 5, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amesema watu 12 wanashikiliwa kwa tuhuma za kuwalawiti wanafunzi hao.
Amesema kukamatwa kwa watu hao kulitokana na taarifa alizozitoa mwanafunzi huyo wa sekondari ya Hai Day ambaye alikutwa ametupwa kichakani.
Amebainisha kuwa mwanafunzi huyo aliokotwa na raia mwema na alipohojiwa alieleza kuwa walikuwa wanafunzi wengi waliofanyiwa kitendo hicho.
Amesema baada ya kauli hiyo wanafunzi hao walitafutwa na kukubali kuwa walilawitiwa, ni
wanafunzi wa shule ya sekondari Hai Day na Boma, wengi ni wa kidato cha pili na walikuwa zaidi ya 17.
“Tuliwatafuta wanafunzi wote na wamekubali kuwa wamekuwa wakitumika na watu tofauti tofauti na uchunguzi unaendelea ili kuwatia nguvuni,” amesema.
Amesema waliotajwa kufanya kitendo hicho ni madereva bodaboda, bajaji na wafanyabiashara wa santuri (CD).