serikali pumbavu inayodhani inakuza uchumi kwa kupandisha kodi. kwa kifupi kila sehemu waliyopandisha kodi kumetokea matokeo hasi, kuanzia madini, miamala ya simu, utalii e.t.c
yale ni maoni ya zito ambayo sikubaliabi nayo kwa kila kitu, anahaki ya kutoa maoni yake. lakini ukweli unabakia kuwa ongezeko la kodi linaua uchumi, wenzetu wanapunguza kodi kuvutia mitaji sisi tunaongeza
Nyie ndie watu wa ajabu kupita maelezo. Unadhani kodi huwa inaongezwa kiholela bila kuangalia impact? Haya sasa, umeambiwa mtu aliekuwa analipa kodi ya sticker 300m kwa mwaka kaongezewa nae kaamua kuachana na hizo stickers. Sijui kama utaelewa, ila ngoja nikupe scenario:
Kampuni A inahitaji stickers kama marketing tool, marketing research yao inawaambia kuwa wasipotumia stickers watauza 600m, na wakitumia stickers (spending 300m) wataongeza mauzo kufikia a maximum sales potential yao 1B. Ukiwaongezea kodi ya sticker ikafikia 500m then watakuwa hawana haja ya kutumia stickers kwa sababu the incremental sales revenue associated with additional costs using stickers will benefit less. So unless wewe ni ccm, obviously hutakuwa na sababu ya kulipa ile addional tax - ng’oa stickers ili ubaki na minimum achievable sales of 600m without stickers. Umeelewa japo kidogo au nilikuwa natwanga maji kwenye kinu?
Btw:
ATCL hawajawahi hata kule kutengeneza financial statements tangu 2015 - na hizo za 2014 hazijawa audited bado. Halafu unitarajie nimpigie makofi “kwa kwa kwa kwa” kumshangilia mtu anaeunguza pesa ya umma eti kufufua shirika ambalo wala hali halisi yake ya kifedha kuhusu mali na madeni yake haijulikani (wakati hospitali hazina dawa, shule hazina waalimu wala vitabu, vijijini hakuna maji n.k, n.k, n.k)? Hiyo laana bakini nayo wenyewe. Siwezi kuwa zwazwa wa aina hiyo wakati Mwenyezi Mungu alinipa akili niitumie.
Sio Hao tu hata Panasonic kiwanda cha batteries kilichowekezwa na wajapan pale Tazara since 1962,Mwaka huu wamesepaZao ili kumwachia Jiwe akusanye kodi vizuri bila kelo.
Kazi ipo. Bora sirikaly ingeanika mipango ya kodi kwa wadau waipepete kwanza wapate mrudisho nyuma. Badala yake wanajifungia na kufyatua vitu vinavyoishia kugota matopeni kabla kuanza mwendo.
Mbolea ya kukukuza uchumi Tanzania ni kupunguza kodi tu, hii atawezesha watu kutengeneza mitaji na kukuza iliyopo, wajaribu, kufanya vat 5% and Cop10% total 15% waondoe tozo na ada zingine, wahakikishie wafanya Biashara hakuna kupandisha kodi zaidi ya 2% bila makubaliano kwanza. Baada ya miada 5, viwanda, Biashara na ajira, zitakua kila kona, na hakuna njaa.