Ushuani nimeishi udogoni, uswazi ukubwani kwa sana…
Ushuani kuna akili za darasani, uswazi ni chuo cha maisha
Watoto wa uswazi ni more creative linapokuja suala la maisha kuliko ushuani
Ushuani hatuna vituko kama uswazi sema huku tuna miss ule ushirikiano kama wenu huko kwamba mnaweza kushare vitu na jirani, huku kila mtu na lake ata jirani humjui labda unajua gari lake tu
Nilipokua mdogo ndo niliishi ‘ushuani’ kuhusu msos nilikua nachagua sana chakula, maharage nakunywa mchuzi tu mchuzi ukipika nachambua vitunguu natoa nilikua nikiona pilipili hoho kwenye mchuzi nishashiba, mihogo sikua nakula viaz sili yan nilikua kama fito nilipokuja kuishi maisha bila ya baba ndio nilipojua uswaz kukoje sikuchagua tena nabugia tu