1)Alisha amuru Mungu,tunapaswa kuungana
Tena tuwe na uchungu,pale tukikwaruzana
Na tuyaache majungu,tusije pata laana
Yatupasa kuungana,waisilamu ni ndugu.
2)Na dini yetu ni moja,kwanini tunatengana
Maadui watungoja,sisi tuanze zozana
Wavunje wetu umoja,wao wazidi shikana
Yatupasa kuungana,waisilamu ni ndugu.
3)Kwanini Shia na Suni,Arabuni mwauana
Mnapigana kwanini,wenyewe mwamalizana
Wapi yasema Qurani,mlipaswa kuchinjana
Yatupasa kuungana,waisilamu ni ndugu.
4)Tusomeshaneni dini tupate kusikizana
Turejee vitabuni,huko tutaelewana
Tuingie darasani,na kwa hoja kushindana
Yatupasa kuungana,waisilamu ni ndugu.
5)Na Dua tuombeane,tuache kuchukiana
Na wala tusigombane,Bali kuelimishana
Mapungufu tujuane,daawa tukipeana
Yatupa kuungana,waisilamu ni ndugu.
SHAIRI-WAISLAMU NI NDUGU.
MTUNZI-Idd Ninga,wa Tengeru Arusha.
+255624010160 [email protected]