Copy pasta kutoka pale kwa Zukabaaga
SHAIRI: Vifaranga Vya Kompyuta
Wageni waheshimiwa, ma’observer
Wakenya, wenye kutumia mwakenya
Na wapiga kura wenzetu
Jina letu ni Vifaranga Vya Kompyuta
Kutoka shule ya taifa la Aiii Bisi
Sanduku la posta ni milioni nane
Eluf mia mbili na tatu, Bomas!
Tuko tayari kuwakariria shairi
Lenye kichwa Vifaaaaaa ranga
Lililotungawa na Larryyyy Liza!
Kaaaaaribuni! Tamanikeni!
Baba keshasema, sisi ni vifaranga
Kigeugeu kakiri, sisi sio makanga
Mluhya akasema, kitini tunakaanga
Kama kompyuta, sisi tunafanananga
Kama unatukaranga, tutaenda kwa mganga
Kanaani hatujafika, hata vindu vikichenjanga
Baba na mama yetu, ni Chebu na Chiloba
Letu jina la familia, makinika na Kompyuta
Kompyuta mapenzini, kompyuka katutaga
Kompyuta katuangua, kompyuta katutoa
Kortini tukutane, tamati shairi nitie nanga
Kompyuta itagayo, hatukubali tena nchini
Hamsini na nne, arobaine na nne
Hujuma sio haba, vifaranga vyetu tupate!
Asanteni.