Unafiki wa viongozi wa kiserikali ndani ya nyumba za ibada kuhusu neno 'kulinda amani'

Huwa nachukia sana viongozi wa Tanzania wanapokuwa kwenye nyumba za ibada wanapotoa matamko yenye kubeba ujumbe wa kulinda amani, neno hili kwao hulitoa kinafiki sana ili kuficha maovu yaliyobeba dhamira zao mbaya dhidi ya taifa hili, huwezi kuhubiri amani bila kusisitiza haki kutendeka kwa jamii wanayoiongoza, tabia hii ya kushindwa kuhubiri haki itendeke na badala yake kuhubiri amani imehamia hata kwa viongozi wa dini wawapo kwenye nyumba zao za ibada.

Hakuna hata kiongozi mmoja wa kiserikali anayesimama ndani ya nyumba za ibada na kusisitiza haki ndio msingi wa amani popote pale duniani, kila mmoja anayesimama anasisitiza tulinde amani, na sijui amani italindwaje bila haki kuwepo, wanafanya haya kuficha dhamira zao mbovu kwa baadhi ya makundi ya kijamii hapa nchini

Dini katika zama hizi zimekuwa pango la wanyang’anyi kwenda kufichia maovu yao mbele ya jamii, viongozi wa dini wanashindwa kabisa kuwakemea hadharani kwa matendo yao machafu kwa wanao waongoza, na badala yake wakiwaona viongozi wa kidunia wakiingia kwenye nyumba zao za ibada hukenua meno yote 32 ya mtu mzima kuashiria kwamba anaona kama katembelewa na malaika, taifa hili limekwama tuwakatalie hadharani hawa viongozi wanafiki wa kidunia na wa kiimani

Kiongozi anasema hadharani kabisa kuwa Mimi haki za bimadamu siyo kipaumbele changu, na huyo huyo anasema atawashughulikia wale wote wanaomkosoa na akakazia kabisa kuwa anashangaa kwanini hadi leo bado wanaishi, kauli hizi ni chache sana kati ya kauli nyingi zinazohatarisha uhai was taifa hili zinazotolewa na hawa viongozi wa serikali ndani ya nchi hii, na hakuna kabisa kiongozi yeyote wa dini aliyewahi kuonya matamko ya kijinga kama haya yenye kila dalili ya kuligawa taifa lilijengwa kwa misingi ya umoja na mshikamano

Taifa hili linahitaji mapinduzi makubwa sana ya kifikra ili tuondokane na huu ushabiki uchwara uliojikita ktk jamii yetu ambao madhara yake tumekuwa tukikumbana nayo mara kwa mara

Neno Amani huwa haliubiriwi kwa bahati mbaya mkuu, ni kuwatengenezea watu uoga ili waendelee kuwa maboya na wasidai haki zao.

Ha

hakika mkuu

Huyu jiwe ni rais Wa ovyo tokea nchi hii ipate Uhuru.hakujiandaa wala hajui haki za watu anaendesha nchi kama familia yake .hajui amani kama ni tunda LA haki.Kule kwa maaskofu amegonga mwamba sasa amekimbilia msikitini

Hatari sana mkuu

Jamaa ukimuona amepiga magoti na kuifunga ile mikono yake akiwa Kanisani utafikiri hakupanga TL kupigwa risasi siku ile.

inasikitisha sana mkuu ,tuwaombee kwa Mungu ili wabadilike hakuna namna nyingine zaidi ya maombi!

Exactly!

[SIZE=5][COLOR=rgb(184, 49, 47)][FONT=arial]siongelei unafiki wa wamasiasa bali nakerwa sana na unafiki wa vioongozi wa dini, mim na siasa mbalimbali ila sipendi kabisa kiongozi wa dini avunje miiko ili kumbeba mwanasiasa fulan[/FONT][/SIZE]

Juzi alienda kuwapa milioni 10 za ujenzi wa msikiti…jana masheikh wakatoa tamko lile lile walilomezeshwa na Magufuli.

Upande huu mkuu usije ukautegemea(BAKWATA) labda Sheikh Ponda.

Karibu mkuu.

No, huko umeenda mbali sana. You are wrong. Never generalize.

Wanataka amani ili watumbue kwa raha kodi zetu, pasipo amani hata hizo walizoiba hazitakuwa na maana kwao…hakuna ambaye hataki amani…ila itapendeza zaidi vikienda sambamba, AMANI na HAKI.

Definitely can not include KKKT, RC… never and some of our colleagues on the other side! BUT some like Malasusa has to be condemned!

Hawawezi kuhubiri haki na usawa kwa sababu maagizo kutoka juu ni kuhubiri amani bila haki… hawana jinsi…

Ni kwamba siyo toa haki na usawa ili kulinda amani lahasha… badala yake ni…

Linda amani hata kwa kuminya haki na kutotoa usawa…

Cc: @Mahondaw

Ni kweli mkuu. ni ishu ya kushangaza sana kwamba viongozi wa Tanzania wanaitumia amani kublackmail wananchi!. kwamba ukifanya hivi au vile amani itaondoka, hapo mwananchi anarudi nyuma.

Mengine hayaelezeki

Mahubiri ya amani pamoja na ushirikina wao wa mwenge.

Bado tuna safari ndefu sana, tusikate tamaa

Hakika mkuu nimarufuku kukata tamaa