Uliza chochote kuhusu 'Aqidah' ktk uislamu..!!!

بسم الله والصلاة و السلام على نبى و على آله و أصحابه وسلم

Sambamba na kichwa hapo juu, hoja inajitosheleza!! Basi ni matumaini yangu wajuvi na ama wenye ghera ya kutaka kujua dini yao hususani mambo ya 'aqiyda watatiririka hapa!!
الله ورسليه أعلم…
AHSANTENI na karibuni…!!

Aqiyda ni nini?

Mtoa mada tafadhali tusaidie hili.

Tupo elim shehe

‘Afuwan…!!’ Niko safarini ila nitajitahidi kujibu kadiri ya wasaa.!!

Assalaam alaikum warahmatullah wabarakaatuh…

Afuwan ndg zangu, nilikuwa safarini kidogo hivyo nilishughulishwa sana kiasi sikuweza kujibu chochote ktk maswali yenu japo nilitamani kufanya hivyo, naomba mnisamehe na kuanzia sasa kwa makadirio yake Allah sub-haanah wata’ala tutaendelea…

Kwa kifupi,
العَقيدة فهي الأمور العلميّة التي يَجب على المُسلم أن يَعتقدها بقلبه.
Aqidah ni mambo ya kielimu (ktk uislam) ambayo inamuwajibikia muislam kuyaitakidi kwa moyo wake.

    [U][B]Mambo yenyewe ni:-[/B][/U]

[ol]
[li]Kumuamini Allah[/li][li]Kuamini malaika wake[/li][li]Kuamini mitume wake[/li][li]Kuamini vitabu vyake[/li][li]Kuamini siku ya Kiama na[/li][li]Kuamini Qadari kheri na shari zinatoka kwa Allah[/li][/ol]

Naam, karibu ndugu…

Shukran nimekuelewa ndugu

kitu gani kitafanyika siku ya kiama na baada ya hapo kwa mujibu wa imani yenu ni kipi kitaendelea?

kwa sababu nguruwe kwa mujibu wa imani yenu ni haramu( kwasabb imetajwa wazi) je matendo kama kuchoma udi na kuamsha majini kwa kutumia maandiko yanayo endana na imani yenu si haramu?

kwa sababu sigara haikutajwa waziwazi kuwa haram na wapo maustaadh na viongozi wengine wa imani yenu wanatumia tu vizur tuite ni halali?

nitaendelea

Siku ya Kiama siku itakayoambatana na matukio mengi mbali mbali ktk
kuelekea hukumu.
Neno Kiyaam/Kiama ni Kisimamo hivyo imeitwa Kiama kwa mnasaba wa tukio la Kusimama. Hivyo kwa uchache kutokana na swali lako miongoni mwa matukio ya siku ya Kiama ni
[ol]
[li]Ufufuo, baada ya viumbe vyote kufa baada ya kupulizwa baragumu la kwanza na muda mwingi kupita, litapulizwa baragumu la pili kisha viumbe vyote vitafufuliwa. وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّهُ ۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ (68) na litapulizwa baragumu kisha vitakufa vilivyomo ktk mbingu na vilivyomo ktk ardhi ispokuwa atakayempenda Allah, Kisha litapulizwa tena, tahamaki (viumbe vyote) vitasimama vikiangalia…!![/li][li]Kiyaam/Kisimamo. Baada ya hapo kutakuja kisimamo, watu watasimama juani kwa muda mrefu sana mpaka watu watawaendea mitume kumuomba Allah alete hukumu. Hapo pia kuna mambo mengi yatapita.[/li][li]Swiraat/Njia. Watu watapitishwa ktk njia nyembamba mno ktk moto wa Jahamnam, wenye makosa watatumbukia na wenye kheri watapita.[/li][li]Hesabu. Sambamba na kupita ktk njia nyembamba juu ya moto wa Jahamnamu ila watu watahesabiwa amali zao, atakayezidi maasi aingie motoni na atayefaulu aingie Peponi. [/li][SIZE=6] فَأَمَّا مَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ [/SIZE]Basi ama yule mizani yake itakayokuwa mizito[SIZE=6] [/SIZE]

فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَاضِيَةٍ (7) Huyo atakuwa ktk maisha yenye kuridhiwa (peponi)

وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ (8) Na ama yule mizani yake itakayokuwa myepesi

فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ (9) Huyo mama yake (Makazi yake yatakuwa ktk moto wa) Haawiyah.
[li]Pepo. Mwisho ni watu kuingia peponi humo wakae milele na waruzukiwe neema za kila namna.[/li][/ol]

kwa sababu nguruwe kwa mujibu wa imani yenu ni haramu( kwasabb imetajwa wazi) je matendo kama kuchoma udi na kuamsha majini kwa kutumia maandiko yanayo endana na imani yenu si haramu?

kwa sababu sigara haikutajwa waziwazi kuwa haram na wapo maustaadh na viongozi wengine wa imani yenu wanatumia tu vizur tuite ni halali?

nitaendelea

Kama nimekuelewa umeuliza kuhusu mambo matatu.

  1. Uharamu wa nguruwe, Hapa umethibitisha kwakuwa jambo lenyewe lipo wazi kwa mujibu wa msingi wa Imani yetu, ni kwwli uharamu wa nguruwe ni jambo ambalo halina shaka. Ni haramu hasa!!

  2. Hapa umezungumzia matendo ya kuchoma udi na kuamsha majini kama nayo ni haramu kwakuwa ufanikishaji wa vitendo hivyo kunatumika maandiko yenye kunasibika na imani yetu. Ndg yangu ktk Uislamu hakuna kitu kuchoma udi, kuamsha majini ama matendo yoyote yanayofanana na hayo kuwa ni sehemu ktk mafundisho ya dini, hakuna. Na kama kuna mahali unaona tukio kama hilo linafanywa kwa mnasaba wa dini basi ni jambo la kimakosa na mtendaji atawajibika peke yake.

  3. Umeelezea juu ya watu wa kuitwa Mashekhe/Maustadh ambao wanavuta sigara ukatatizika kwamba je kwakuwa sigara haikutajwa kama alivotajwa nguruwe, na kwakuwa hao watjwa hapo juu miongoni mwao wanatumia hiyo kitu inafaa kusema ni halali?

Kuhusiana na hilo ndg yangu nikufahamishe tu kwamba Uislamu si dini inayofata matendo ya mtu, bali watu ndio wanatakikana wafate matendo ya uislam. Sio sigara tu, ukiona shekhe, ustaadhi au muislamu muumini wa kawaida anakula nguruwe, anavuta sigara, anakunywa pombe, anacheza kamari, anazini au jambo lingine lolote la kimakosa hayo ni ya kwake huyo huyo mtendaji, Uislamu uko mbali naye na anadhima ktk uovu wake huo.