Mara nyingi watu wamejaribu kujifananisha na watu wengine wakidhani ndiyo njia sahihi ya kufikia malengo au mafanikio wanayokusudia.
Si kosa kutaka kufikia kiwango cha mtu fulani katika ndoto uliyonayo kwa maana ya “level” ya mafanikio lakini si rahisi kupita njia zake kama ilivyokuwa ili kufika hapo.
Unaweza kufika katika “level” ya kuwa Bilionea kwa njia tofauti kwa sababu wewe ni wewe na huyo unayemuiga ni mtu tofauti na wewe na hivyo kusudi la KIMUNGU juu yenu ni tofauti.
Kila unapoiga njia za mwenzio ndivyo unavyopishana na kusudi lako kwa sababu unatumia njia isiyokusudiwa kwako. Mungu anapokupa Ndoto yako Lazima atakupatia na jinsi ya kuiendesha Ndoto hiyo kuelekea Mafanikio yaliyokusudiwa. Tatizo letu ni kwamba hatupo ama hatukai vizuri na Mungu wetu ili kupata njia sahihi na badala yake hujiegemeza kwa wanadam wenzetu na kuwategemea kwa asilimia zote.
Tutamani mafanikio lakini tusiige kila kitu. Ipo sauti inakusemesha ndani yako, inakuelekeza njia bora ya kufikia malengo yako lakini huisikii, unaiacha na kuchukua ya mwenzio ambayo wala huna ndoto nayo. Haitakusaidia kitu, inaweza kukupoteza kisha ukamtangaza mwenzio vibaya pasipo kujua kwamba ulitaka kupita mlango si wako.
Wakati wote hakikisha unakuwa wewe na Ndoto yako, elimu uliyonayo na uyasikiayo kwa wengine yafanyike kuwa uboreshaji na kukuimarisha kubaki kuwa wewe. Wewe ni HALISI kwa kusudi lako na kila mtu ni halisi kwa kusudi lake…
Mara nyingi watu wamejaribu kujifananisha na watu wengine wakidhani ndiyo njia sahihi ya kufikia malengo au mafanikio wanayokusudia.
Si kosa kutaka kufikia kiwango cha mtu fulani katika ndoto uliyonayo kwa maana ya “level” ya mafanikio lakini si rahisi kupita njia zake kama ilivyokuwa ili kufika hapo.
Unaweza kufika katika “level” ya kuwa Bilionea kwa njia tofauti kwa sababu wewe ni wewe na huyo unayemuiga ni mtu tofauti na wewe na hivyo kusudi la KIMUNGU juu yenu ni tofauti.
Kila unapoiga njia za mwenzio ndivyo unavyopishana na kusudi lako kwa sababu unatumia njia isiyokusudiwa kwako. Mungu anapokupa Ndoto yako Lazima atakupatia na jinsi ya kuiendesha Ndoto hiyo kuelekea Mafanikio yaliyokusudiwa. Tatizo letu ni kwamba hatupo ama hatukai vizuri na Mungu wetu ili kupata njia sahihi na badala yake hujiegemeza kwa wanadam wenzetu na kuwategemea kwa asilimia zote.
Tutamani mafanikio lakini tusiige kila kitu. Ipo sauti inakusemesha ndani yako, inakuelekeza njia bora ya kufikia malengo yako lakini huisikii, unaiacha na kuchukua ya mwenzio ambayo wala huna ndoto nayo. Haitakusaidia kitu, inaweza kukupoteza kisha ukamtangaza mwenzio vibaya pasipo kujua kwamba ulitaka kupita mlango si wako.
Wakati wote hakikisha unakuwa wewe na Ndoto yako, elimu uliyonayo na uyasikiayo kwa wengine yafanyike kuwa uboreshaji na kukuimarisha kubaki kuwa wewe. Wewe ni HALISI kwa kusudi lako na kila mtu ni halisi kwa kusudi lake
Hayo maneno kwenye bolded letters ni ya kuzingatiwa sana…
Kila mara naota nipo darasani ama wakati mwingine chuoni. Ndoto inanitaka nirudi shule elimu ya juu nimegoma; najua hiyo ndiyo root success yangu ilipo lakini sitaki kukaa darasani mimi; kifupi sitaki kusoma; let it be.
Unaweza kujua root ya talent yako ilipo ila ukawa huipendi na ukaagukia kwingine unakokupenda wakati root ya success yako haipo huko. Ni changamoto kwa tulio wengi.