Duniani kuna tabia ambazo ningumu kubadilika hasa pale zinapokuwa sehemu ya maisha ya mtu. Nimeona kuna baadhi ya watu wanailaumu TBC1 na TV1 kwa kutoa habari na matangazo ya uongo/umbea kwamba watatangaza BURE mechi zote 64 ktk kombe la dunia, kwa mtu mwenye akili timamu na anayeifahamu TBC1 vyema hili tangazo kwake lilikuwa KICHEKESHO kama zile clip za Mr Bean au Joti.
Hivi hawa TBC1 si ndo wale walioshindwa kurusha bunge live kwa kisingizio cha bajeti? Si ndo hawa waliosema rais Trump kamsifia Mh Magufuli kumbe ni uongo? Sasa mtu na akili timamu unaweza kuamini watu wa namna hii eti watarusha mechi 64 bure wakati Channels nyingi zimetamani kufanya hivyo ila budget ikawashinda? Kama kurusha bunge lao ni kitendawili watawezaje kurusha mechi 64 za gharama kubwa?
Haya mambo aliyaweza Tido tu ktk enzi zake.
Poleni sana waliotegemea TBC mimi naomba mniruhusu niwachekeke kwa EMOJI:D:D:D:D:D:p:p:p:p:p mmeingizwa mkenge hahahahaaaahahahaaaa, Wapi Remote yangu ya DSTV…
Mimi mtanzania nipo Tanzania ila naangalia kombe la dunia kupitia Rwanda Tv yaani hawa wanaonyesha live kabisa picha nzuri. Ngogoti anawapenda watu wake aiseee. Bure kabisa
mkuu walivyo mrusha dr slaa na mwenzake kutoka sweden live tukajua bas kurusha kutoka russian n sawa na kutoka ushirombo, pili kuna lile tangazo itv na chanel ten wanasema kbsa “kama sio dstv bas potezea” wanaume tukamwamin yule mzee mweus kama ukuta wa jikon na bichwa lake lililojaa maganda ya karanga na miwa.