Liverpool imeanza tena mazungumzo na Lyon kwa ajili ya kiungo mshambuliaji Nabil Fekir, 24.
Lakini Manchester United pia inamuhitaji mchezaji huyo.
Chelsea inatarajia kumtangaza meneja wa zamani wa Napoli Maurizio Sarri kuwa meneja wao mpya juma lijalo.
Tottenham wanampango wa kumnyakua kiungo mshamuliaji wa River Plate na timu ya taifa ya Colombia, Juan Quintero, 25.
Leicester City wamemteua Jacques Bonnevay kuwa meneja msaidizi wakati Michael Appleton akiondoka.
Mlinda mlango Thibaut Courtois yuko tayari kuondoka Chelsea ikiwa mbelgiji huyo atatimiza ndoto zake kuelekea Real Madrid.
The Blues wanasuka mipango ya kumnyakua mlina mlango wa Roma Alisson, 25 kwa kitita cha pauni milioni 65 wakiwa na mashaka ya kumpoteza Courtois.
Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech, 36, amesema Napoli imeonyesha kumuhitaji lakini yeye ana mpango wa kubaki Emirates.
Arsenal wanajiandaa kukamilisha mazungumzo kuhusu kumsajili kiungo mshambuliaji wa Uruguay Lucas Torreira, 22 kutoka Sampdoria juma lijalo.
Liverpool hawana mpango na kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio, 22, pia mchezaji mwenzake Lucas Vazquez
Juventus sasa inaongoza katika kuwania sahihi ya Sergej Milinkovic-Savic, 23 kutoka Lazio.
Manchester United huenda ikamchukua beki wa AC Milan, Leonardo Bonucci, 31 kutokana na timu hiyo kufungiwa kushiriki mashindano ya ulaya.
Daniele Rugani, 23, wa Juventus amekubali kujiunga na Chelsea.
[ATTACH=full]180834[/ATTACH]