Taifa la Misukule laja

From JF kuliko na waoga!
Kila nikitafakari tanzania ya kuanzia miaka 10 ijayo na kuendelea kwa akili za sisi wazazi wa leo sipati picha kamili watakua watoto wa aina gani na wao watazaa watoto wa aina gani. ila nabaki na jibu moja tuu kitakua kizazi cha hovyo sana.

[ol]
[li]Yaani watakua kama misukule. watakua kama maroboti wanaoongozwa na nchi zingine au na watu wachache watakaobahatika kuishi nje ya nchi zaidi ya hapa Tanzania lakn wakawa ni watanzania. maana watakuwa na akili kubwa kuwazidi hawa watanzania ambao ni kama kuku wa kisasa wamefungiwa akili zao wasiingize chochote zaidi ya kile watawala wanachotaka. cha ajabu na sisi wazazi tumekubali haya yaendelee.[/li][/ol]
Natamani tufute vyama vyote labda akili ndio itaturudia na kujiona sisi wote hii ni tanzania yetu. ila kwa sasa naona tumepotea na sijui lini tutarud kwenye msitari. maana tumeigawa Tanzania katika makundi kuna watu ambao kila kitu wanapinga na kuna watu kila kitu wanaunga mkono. haya ni makosa makubwa sana. watanzania hebu tuamke kuijenga nchi yetu kwa vizazi vijavyo.

Hebu tutafakari jambo moja tuu ambalo serikali imetuletea na kuna watu wanaunga mkono bila kujua athari zake kwao na kwa kizazi kijacho.

TAKWIMU.

Serikali imeleta sheria kali ya takwimu eti watu wasitoe takwimu yeyote mpaka kwa kibali chao. yaani ikosee harafu ikupe kibali cha kwenda kuikosoa kwa kuweka takwimu zingine kwa hisani yake . harafu kuna watu wanasema ndiyoooooooooo!!! pumbavu kabisa.

Yaani mfano tuna shule laki moja wanatwambia tumegawa vitabu milioni 2 katika shule zote lak moja. sasa mimi ni mwananchi au mwalimu ninajua kabisa katika shule ya ujiji vitabu hivyo havipo. nampigia simu mshikaji wangu yupo mbeya huko kuuliza kuhusu vitabu hivyo anasema vipo viwili tuu. Tunafanya uchunguzi wetu na kubain wilayani kwetu penye shule mfano kumi kulitakiwa kuwe na vitabu 200 ila kuna vitabu 20 tuu ambavyo vilistahili kuwa katika shule moja kwa mujibu wa takwimu ya serikali kwamba imegawa vitabu mililion 2 katika shule laki moja.

Sasa tukiwaambia serikali waongo vitabu havipo mashuleni eti ni kosa natakiwa nifungwe miaka mitatu au nilipe faini milion 10. Badala ya serikali kuja na majibu sahihi ili kuniweka sawa wao wananiandalia jera. harafu kuna watu wanasema serikali iko sawa kuleta hiyo sheria. nawaambia nyie wafia chama maana sio wafia Tanzania mnaandaa kizazi cha hovyo sana huko mbeleni. yaan tutakua na kizazi cha ndio kila kitu. tutakua taifa la mazombi taifa la misukule taifa lenye watu kama maroboti naam taifa la kuku wa kisasa.

Dunia iko hivi ilivyo kwa vile kulikua na mawazo mbadala. nyie mnaounga kila kitu tulipowaambia kukosoa ni afya katika nchi mkasema no kukosoa mwache rais wetu afanye kazi. haya na sasa ameleta sheria akisema tumepata trilioni 30 sema sawa akisema tumetumia trilioni 32 usimuulize mbona hesabu inatofautiana wewe sema sawa tu. akisema tumetumia trillion 28.5 usimuulize 1.5 iko wap. akisema nimepeleka Zanzibar ww sema sawa tuu!! yaan misukule nyie yaan napata hasira sana nikitafakari haya.

Watoto wetu watazaliwa na kutukuta sisi tukisema ndio kila kitu watajua ndio utaratibu na wao wataiga mwishoe tutakua na kizazi cha hovyo huenda kuliko taifa lolote duniani.

Hatujachelewa tuamke tuwaambie hawa wanasiasa hata sisi akili tunazo . Mungu aliye wapa wao akili hata sisi katupa . wasifikiri kwa niaba yetu hata sisi tunaweza kufikiri. Wafanye tulio watuma wakafanye sio waliojiamulia. kukabidhi akili yako iendeshwe na mtu mwingine huo ni utumwa mbaya kuliko wa kikoloni.

Vitu vya ajabu saaana.

Yaani mpaka tunatia huruma!

Ngoja tuone… tunasikitisha sana…

Cc: @Mahondaw