Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salam imefanikiwa kumsajili mshambuliaji raia wa Rwanda, Meddie Kagere kutoka Gor Mahia ya nchini Kenya.
Mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake na Gor Mahia unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka huu, amejiunga na Simba akiwa mchezaji huru na anatarajia kuonekana akiwa na jezi ya Simba kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki inayotarajia kuanza kutimua vumbi hapa nchini June 28.
Aidha, imeelezwa kuwa Kagere amesaini kwa dau la dola 50,000 sawa na zaidi ya shilingi million 110 za kitanzania huku mshahara wake ukitajwa kuwa ni dola 5,500 ambazo sawa na zaidi ya shilingi milioni 12 zakitanazania.
Wengine waliotambulishwa ni pamoja na Serge Wawa na Deogratius Munishi waliosajiliwa hivi karibuni, pia Adam Salamba, Mohamedi Rashid na Marcel Kaheza ambao walisajiliwa mapema wakati dirisha la usajili lilipofunguliwa.
[ATTACH=full]180318[/ATTACH]