Shoka

Usiku Sultani Shahzaman akakumbuka amesahau zawaidi muhimu aliyodhamiria kumpelekea kaka yake. Basi bila kuonekana na mtu, akatoka hemani mwake, akarejea kwenye kasri lake.

Alipoingia ndani, la haula! akamkuta mkewe amekumbatiwa kimapenzi na mtumwa wake mmoja! Kuona vile, akapigwa na butaa; haku-weza kuamini yale aliyoyashuhudia pale penye sofa!

Akafikiri, “Kama kitendo kama hiki kinaweza kutokea wakati sijafika mbali, iblisi huyu atafanya nini nitakapokuwa mbali?”
Hapo akafuta upanga wake, akawaua wote wawili pale