Shairi

Mgeni Mheshimiwa,
Waamuzi,
Mabibi na mabwana.

nikiwakariria shairi liitwalo “Ramba”!!
Karibuni.

Nilichokitetea, kinaniramba!
Kimeniramba sukari,
Kinaniramba Unga,
Chaniramba mafuta,
Kinaniramba na chumvi,
Kimeramba mahindi,
Kinaniramba tu!

Mlichokishangilia, kinawaramba!
Kinawaramba njiani,
Kinawaramba nauli,
Kinawaramba karo shuleni,
Kinawaramba mishahara,
Kinawaramba mifuko,
Kinawaramba tu!

Tulichokisifia, chaturamba,
Kinawaramba Sadaka,
Kinawaramba dukani,
Kinawaramba kwa baa,
Chawaramba kanisani,
Kinawaramba zaka,
Kinawaramba tu!

Kinaramba wafuasi,
Kinaramba na waasi,
Kitawaramba waalimu,
Kinawaramba madaktari,
Kinawaramba USHURU,
Kirambe ‘fedha za nyumba’,
Kinaturamba tu!

Tulichokipigania, cha ramba,
Kinawaramba makanga,
Kinawaramba mahasla,
Kinawaramba wakulima,
Kinaramba Askari,
Kinaramba kila mtu,
Kinaturamba SOTE!

Ahsanteni

ii ujinga pelekea assimio lunatic mizee mijinga @gashwin ile kijiji ya wazee

Wee mzee @uwesmake tafta chap akupige chuma hadi ushondeke

hilo ni shairi guni :D:D

halifuati kanuni zozote za ushairi.

Shairi iliandikiwa ndani ya msedes usiku.:D:D

images.jpeg

Kubaff, we Mzee rika yangu.

Walah Bin Walah would be proud of that effort … :D:D

Kuramba au kulamba??

Lugha Ya Kiswahil ina Lahaja tofauti …
Kuanzia Ki-Amu hadi Ki-Ngazija

Kwa Mfano :-
Njoo hapa - Ndoo hapa