Samaki sasa kama Madawa ya kulevya(geita)

Kwa sasa nipo hapa mjin kwa siku kadhaa, raia na wakazi wa hapa wamekuwa wanapata shida kubwa sana hasa kwenye kuuza samaki,

wakina mama wanakamatwa na kupigwa pingu, asubuhi ya leo nmeshuhudia ktk soko la mbugani/joshoni kinamama wanakamatwa na kupigwa pingu, imetokea tafulani kubwa,

Hao jamaa wa mali asili wanakuja na pigu kama wanakamata majambazi au wauza madawa ya kulevya, najiuliza hivi kwel viongozi wa mali asili na uvuvi wamekuwa wazembe kiasi cha kushindwa kutumia diplomatic way?

Inamaana mpka samaki anafika sikoni wameshindwa kumzuia huko anakovuliwa mpka wanamkamata mama ambae anatafuta mkate wake wa kila siku?

Wameishiwa mbinu kiasi cha kuwaonea hawa wakinamama walio na mikopo midogo ili wajikwamue?hivi kwel serikal nzima imeahindwa kuja na mbinu shirikishi ya kuwasidia watu wa geita na maeneo yanayovua?

Nmeaikia jimbo na presidor huko hawakamati na wanakotoka mpina(waziri) je hawa raia wa geita, mwanza na musoma ndo wahanga?

Rais wangu fika mahali waonee huruma hawa watu, itaenea chuku buree,watu mlio karibu na ptesidor mwambieni kuwa kunasiku atashihudia maafa ya wavuvi wa samaki, wafanyabiashara na hao wanaojiita maafisaaa wa mifugo…

Niombe tu, kama samaki hawajazuiwa kenya, na uganda kwa nn sis tunawazuia wakati samaki wanasafri na hawana mipaka?

nasubri majibu ila msinihukum kwa kusema ukweli, msema ukweli ni mpenzi wa Mungu…

Serikali ya wanyonge, lazima wanyongwe!!