Kweli umuhimu wa kitu huonekana pale kinapokosekana. Nimegundua mambo mengi tuliyokua tunalalamika JF kuonewa na mods humu KT yapo ila hatuyafanyi either kwa kuogopa sheria za JF au mazoea tuliyozoeshwa na JF mods,baadhi ya mambo hayo ni kama vile:
1.kuanzisha nyuzi nyingi zenye maudhui sawa. Mfano mzuri ni jukwaa la JF sports ambapo kuna uzi mmoja tu unaongelea masuala yote ya world cup,huku wenyeji wetu jukwaa lao la sports wapo free kuanzisha uzi kwa kila mechi ya world cup na nyuzi haziunganishwi.
2.lugha mbovu,wenzetu wanajiachia watakavyo wanatukana wee ila sie tunajishtukia kwa kuogopa ban
Kuchat na mods,mfano kuna mod mmoja humu nilimuona anachat nyuzi za chit chat tena akadaka na mchuchu kabisa nadhan ilibaki tu kuzinduana hahah,hee niliogopa na kuona humu hatari maana tushazoea JF mods hawachat kwa kujiachia na members. Ila baada ya muda nikazoea.
Ligi za ubuyu,mfano da trump kakinukisha huko insta hadi kuringishia soon atavalishwa pete ila huku watu kimyaa wamepotezea kama vile hawaoni kinachoendelea
Hahahaha tatizo una haraka babu kijana soma vizuri,mod kadaka mchuchu it means ni kijana mwenye manguvu yake,kuwa makini oohoo mwenyewe akiona utakula ban,ban ya ugenini inaumaaa
Nimekuelewa sana… hapa nimekuomba ufanye utafiti uone kama kuna kamod kamchuchu nifanye vitu vyangu. Hakika hutakumbana na kitu kinaitwa Ban kwa hisani ya babu yako mimi mtakatifu
Ustaarabu tunao sana na kingine ni mazoea.
Wenzetu hawa washazoea kutukana,ukipitia nyuzi zao utaona wengi comment zao zina matusi,uaishangae ukakuta mtu kaitwa ng’ombe ama ngamia hahaa!
Jf ukiita hivyo ban hiyo hapo mlangoni
Mods wao ni wapole sijui ama ndo wamezoea wanaona kawaida tu,kuna mtu kaweka avatar hiyo nikasema paw angeiona anakuzawadia ile yao yenye maneno ya red
Umeona eh! huku kujirusha kwa raha za wachangiaji mambo nje nje ila kwenye matusi huku wako wazi sana ila napenda kwenye siasa unachoandika kinabaki hivyo hivyo huna wasi wasi wa MOD gamba kuja kukifuta, kubadili ulivyoandika na hivyo kupoteza maana ya kile ulichoandika. Ila yale mavitu yetu huku kwa sasa nimeshindwa kupost sijui kwanini. Kule JF ni mwendo wa copy na kupaste huku inagoma HOLAAA sijui tatizo nini.