Mwenye wimbo huu auweke hapa jukwaani tafadhali..!!

Kuna wimbo fulani wa Taarabu zamani kidogo, sikumbuki uliimbwa na nani kwakuwa sio mpenzi wa miziki miziki ila kipindi hicho ulihit sana kiasi uliteka na kukonga nyoyo za wengi nikiwemo mimi, ambapo hapa nitaeeka baadhi ya maneno yanayosikika ktk huo wimbo ili iwe rahisi kuukumbuka na hivyo mwenye kuwa nao auweke jukwaani.

[SIZE=3]“Nilidhani nimechanda na wewe ni pete yangu, nikawa ninakupenda kukuona u-mwenzanguu…!!”
“Kumbe nimefuga donda lilowashinda wenzangu, ukawa wagawa tenda hata kwa rafiki zanguu…!!”[/SIZE]

[SIZE=3]“Si mtu wewe ni sanda, wengi wanapongezana, wanavokugombania kama mpira wa konaa…!!”[/SIZE]

subiri wazanzibari waje

Kaimba y Star

Kaimba Aly star?

Ama kweli mzazi wako alokulea kala hasara
mtoto wa kike unamambo ww, unamambo ww unambo
Due!!! hata Mimi naupenda sana

Asante ngoja nami niusakue

Mzuri kweli

mimi naomb wa kuru james mtoto wa dandu ft madiluu system mamuu, huu wimbo hata uufuate makao makuu ya google huupati og labda kama wameuweka hv karbun, naupenda sana

Watu wa Mwambao utawajua tu

Wimbo unaitwa Hauvumi lakini umo, umeimbwa na Ally Star au Ally Hemed. Ingia Youtube, andika Ally Stars TOT - Hauvumi lakini umo.

Hahah

Ally Star “fundi” alikuwaga “mtu wake” Nasma Hamis “Kidogo” RIP

Hii browser ya kichoko sana
Kuna wimbo nautaka Sasa napandisha
Chorus yake nashindwa