Mussa Azzan Zungu awa Spika wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Achaguliwa kwa kura 378 kati ya kura 380 halali

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limefanya uchaguzi wa kumchagua Spika wa Bunge la 13. Kikao hicho kinaendeshwa na Spika wa muda William Lukuvi, akisaidiwa na Katibu wa Bunge Baraka Leonard. Jumla ya Wabunge 383 wanapiga kura.

Katika uchaguzi huu tutakumbuka kuwa Spika wa Bunge lilopita, na Mbunge wa Uyole, Tulia Ackson alijondoa katika kuwania nafasi hiyo katika ngazi ya Chama ikiwa ni baada ya kuwa ameshachukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kuwania nafasi hiyo.​

Wagombea Wawasilisha Sera Zao

Veronica Charles Tyeah kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) aliainisha vipaumbele vitatu vikuu iwapo angechaguliwa: kuhakikisha usawa ndani ya Bunge, kulifanya Bunge kuwa chombo kinachoweka wananchi katikati ya maamuzi yake na chenye sauti inayosikilizwa na Wananchi, pamoja na kubadilisha kambi ya upinzani kuwa “kambi rasmi ya majadiliano” ili majadiliano yawe na tija zaidi kwa taifa.

Alisisitiza kaulimbiu yake ya “Taifa Kwanza, Vyama Baadaye”, akihimiza umoja unaovuka mipaka ya vyama vya siasa kwa ajili ya kujenga taifa lenye usawa na mafanikio. Tyeah pia alimsifu Rais Samia Suluhu Hassan, akimtaja kuwa mfano wa kuigwa aliyempa ujasiri kama kiongozi mwanamke.

Anitha Alfan Mgaya kutoka Chama cha National League for Democracy (NLD) alijitambulisha kama mtaalamu wa maabara na aliyewahi kugombea ubunge Jimbo la Kibiti. Aliahidi kuhimiza umoja wa kitaifa, kusimamia haki, usawa, uwajibikaji, na kuwaongoza vijana kutambua umuhimu wa amani, upendo na utulivu. Pia alionesha dhamira ya kuunga mkono ajenda za maendeleo za Rais Samia.

Alipoulizwa na Mbunge Esther Bulaya kutaja makundi manne ya wabunge, Mgaya alikataa kujibu. Mwenyekiti wa kikao, Lukuvi, alisema hakuwa na wajibu wa kujibu kwani wabunge wote ni sawa bila kujali njia walizoingia nazo bungeni.

Chrisant Nyakitita wa Democratic Party (DP) alieleza uzoefu wake mkubwa wa kisiasa, akiwahi kugombea ubunge wa Musoma Mjini katika miaka ya 2010, 2015 na 2020, na pia kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Kanda ya Ziwa. Aliahidi kushirikiana na wabunge kutoa ushauri kwa Serikali, kutunga sheria zinazozingatia maadili ya Kitanzania, na kudumisha nidhamu pamoja na Bunge lenye mwelekeo wa maendeleo.

Wakati akimwaga sera zake, Mbunge Esther Matiko alimtaka kutaja kanuni ya kwanza na ya pili ya Bunge, lakini Mwenyekiti alitupilia mbali swali hilo, akisema hata baadhi ya wabunge waliopo hawazikumbuki kanuni hizo.

Ndonge Said Ndonge wa Alliance for Africa Farms Party (AAFP) aliwapongeza wananchi kwa kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua wawakilishi wao na kumpongeza Rais Samia kwa ushindi wake. Alitumia neno “KIONGOZI” kama kifupi kueleza falsafa yake ya uongozi— Kukubali Kukosolewa (K), Ijue tabia ya watu unaowaongoza (I), Onesha kwa vitendo (O), Nena Kauli thabiti (N), Gawa Madaraka kwa unaowaongoza (G), Ondoa manung’uniko kwa unaowaongoza (O), Zuia migogoro kwa unaowaongoza (Z) na herufi ya mwisho ni herufi (I) maana yake kama nitakuwa Spika nitainua vipato kwa Wabunge ili wakasaidie wanaowaaongoza maana hii I inamaana Inua vipato kwa unawaongoza.

Amin Alfred Yango kutoka Alliance for Democratic Change (ADC), ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, aliahidi kusimamia amani, kushinikiza upatikanaji wa Katiba mpya, na kuondoa kanuni kandamizi bungeni. Alimsifu Rais Samia kwa mageuzi aliyofanya katika usimamizi wa bandari na jitihada zake za kulinda wanyonge kupitia kamati ya kuratibu haki na amani.

Alipoulizwa na Mbunge Esther Bulaya kutaja kanuni kandamizi moja, Yango alijibu kuwa akiapishwa, atasoma kwa undani kanuni za Bunge kabla ya kufanya mapendekezo mahususi ya marekebisho.

Mussa Azzan Zungu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye alikuwa Naibu Spika katika Bunge lililopita na sasa ni Mbunge wa Ilala, alisema atajikita katika kuhakikisha utekelezaji mzuri wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025–2050. Aliahidi kushirikiana na wabunge kuboresha maisha ya wananchi na kudumisha demokrasia.

Alipoulizwa na Ado Shaubu kuhusu mbunge wa Tundulu Kaskazini mchango wa Bunge katika kuimarisha demokrasia na mchakato wa Katiba mpya, Zungu alisema Bunge litasimamia maslahi ya wananchi na kufuatilia mchakato huo hadi kukamilika.

Akijibu swali la Kangi Lugola kuhusu sera yake ya awali ya “Jaza Ujazwe,” Zungu alisema ataongoza Bunge kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa.

Mbunge Sigrada Mligo wa CHAUMMA alimuuliza namna atakavyohakikisha Bunge linatetea wananchi na si Serikali. Zungu alijibu kuwa jukumu la Bunge si kupambana na Serikali bali kushirikiana nayo kwa ajili ya maslahi ya wananchi kwa kuongozwa na dira ya taifa.

Wabunge Wanaendelea na kupiga kura
Jumla ya Wabunge Wateule 383 wamepiga kura kumchagua Spika. Kwa sasa zoezi zinaloendelea ni kuhesabu kura

Matokeo ya kura
Katika upigajin kura; Jumla ya kura zilizopigwa ni 383 na katika kura zilizoharibika ni 3 ambapo kuna Wabunge wamepigia kura Wagombea wawili.

Matokeo ya uchaguzi wa Spika wa Bunge

  1. Mussa Zungu (CCM) - 378
  2. Veronica Charles Tyeah (NRA) - 0
  3. Anitha Alfan Mgaya (NLD) - 1
  4. Ndonge Said Ndonge (AAFP) - 1
  5. Amin Alfred Yango (ADC) - 0
  6. Chrisant Nyakitita (DP) - 0

poo GIF

poo GIF

poo GIF

poo satisfying GIF

loop poop GIF by Mauro Gatti

poo GIF

poo GIF

Happy Ice Cream GIF by T A R V E R

dog poo GIF

Poo Wtf GIF