Msamaha

Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu.

Tunayo manung’uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.

Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi.

Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.

Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza.

Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na siyo mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu.

Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.

Nawatakia siku njema…

SAMEHE, SAHAU, acha maisha yendelee.

huwa sielewi inakuwaje ndugu hawaelewani!!!

Roho ya ubinafsi ndiyo husababisha yote haya…

Mkuu kwa haya mabandiko yako, kweli ww ni bishop. Shukrani.

Napenda kusema nisamehe sijui kwa nini, kuna rafiki yangu huwa ananishangaa, why niko hivi

Ni kwa sababu unapenda uchokozi, hata kama mtu katulia utataka umchokoze tu ili uone povu, bisha!.. :D:D:D

Maneno mazuri sana haya,naomba mwenyezi Mungu anijaze na roho ya kusamehe…

hahahaaa yaani wewe kama unanijua vile,hii kitu ni tangu mdogo nimezoea maana nilikuwa mwoga kupigwa, na nikiomba msamaha siadhibiwi

@Sesten Zakazaka nimekusamehe tu Hajar mieee.

Hahahaaa. Lol. ( ndukiiiiiiii)

Msamehe tu

Asante, unisamehe saba mara sabini hata nikikukosea tena na tena, si ndio maandiko yanavosema Hajar? Sasa watoka nduki waenda wapi weyee? Rudi na mimi nimekusamehe

Hahahaaaa. Lol. Kumbe ulikosa eee. Ndio sababu Hajar anakupendaga jamaani lol. Haya tugange yajayo sasa Sesten.

Na kweli ndivyo yasemavyo hayo maandiko. Hata mleta uzi kasema “Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho”.

Tujifunzage kusameheana tu kwa kweli Sesten.

kabisa Ndugu umesema ukweli mtupu.

Asanteee, basi uje tugonganishe glass za vinywaji kwa ajili ya kusameheana, sasa sijui tutapata kinywaji gani gani huku kambini Kankuma maana togwa haipatikani, au ‘vyombo’ unagonga Hajar?

Hahahaaa. Lol. Itabidi nikutafute aiseee Sesten. Nina hakika mie wa maji na juice tu nitapata humu kwani haviwezi kosekana.

Ila umejua kunionea mie na vyombo wapi na wapi jamaani Sesten?

Wasukuma wa kule Chato wanasema Maaaayooo au Wasambaa wanasema Tate Naneee, Wachaga wanasema 'Yeleeeuuuwiii, Kiiiruuu…nimelikoroga hapo Hajar, dah! Kweli ilibidi nielewe Hajar na vyombo ni mbalimbali kama polisi na bangi, hapa Kankuma juice na maji vipo lakini mamii, usijali karibu

Hahahaaa. Usijali banaaa.

Itabidi Weekend hii nikucheck kwa kweli.

Hajar wewee, ahadi ni deni ujue maana weekend inaisha leo hivooo, sijui nitachekiwa lini:p:p:p

Hahahaaaa. Ila muda bado upo Sesten.

Wacha nikucheck saa hii basi. Teh teh