NA MWANDISHI WETU
Mwenyekiti waCHADEMA, Freeman Mbowe amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kudondoka ghafla alfajiri ya leo kwa mujibu wa wakili wake Jeremiah Mtobesya.
https://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2018/06/18/Mbowe%20new.jpg?itok=qA1srC54×tamp=1529311010
Wakili wa Mbowe, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mteja wake alianguka leo Juni 18 akiwa nyumbani kwake hivyo asingeweza kufika mahakamani kwa siku ya leo.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Wakili Mtobesya ameeleza kuwa Mbowe ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi namba 112 ya 2018 amefiwa na kaka yake Henry Mbowe usiku wa kuamkia leo.
Awali Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiambia mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa Mbowe na wenzake wanane kusomewa maelezo ya awali PH na kwamba wamejiandaa na wako tayari.
Mungu amsimamie huyu baba jamani,anapitia mengi mno.
Wamemwaribia kila kitu chake na kwakuwa ameendelea kuweka ‘ngumu’ wameamua kudeal nae direct.
Mungu wetu aliye mwema anaona yote haya lakini,hawezi kutuacha tukateseka milele…
Ipo siku
Hii si mara yake ya kwanza kutokewa na hali hii. Miezi michache iliyopita alilazwa ICU hapo KCMC kwa hali kama hiyo. Sasa MNH! Soon atalazimisha apelekwe Ubeligiji!