Mapya zaidi yaibuka kukamatwa kwa mfanyabiashara Zacharia

MONDAY, JULY 2, 2018
Mapya zaidi yaibuka kukamatwa kwa mfanyabiashara Zacharia

Kwa ufupi
Meneja huyo alisema baada ya kumaliza kuangalia taarifa ya habari ya saa mbili usiku, bosi wake (Zakaria) aliaga ndipo ghafla watu wawili walitoka ndani ya gari na kumkamata ili kumuingiza kwa nguvu ndani ya gari lao.

By Waandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Tarime. Tukio la kukamatwa kwa mfanyabiashara wa Kanda ya Ziwa, Peter Zakaria limechukua sura mpya baada ya familia na walioshuhudia tukio hilo kutoa maelezo yanayokinzana na Mkuu wa Mkoa.
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Tarime jana, baadhi ya walioshuhudia tukio hilo, akiwemo msemaji wa familia, Samuel Chamete na meneja wa kituo cha mafuta ambako tukio hilo lilitokea, Samuel Athumani walisema taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima inakinzana na ukweli.

“Nilikuwepo na nilishuhudia tukio kuanzia mwanzo hadi mwisho. Wale watu hawakuja kujaza mafuta kwa sababu kituo kilishafungwa tangu saa 12:00 jioni,” alisema Athumani.

[COLOR=rgb(226, 80, 65)]Alisema, “Baada ya kuona gari lao limesimama muda mrefu bila wahusika kushuka, nilimtuma mfanyakazi kuwauliza iwapo wana shida tuwasaidie na wakajibu hawana shida.”

Meneja huyo alisema baada ya kumaliza kuangalia taarifa ya habari ya saa mbili usiku, bosi wake (Zakaria) aliaga ndipo ghafla watu wawili walitoka ndani ya gari na kumkamata ili kumuingiza kwa nguvu ndani ya gari lao.
[B]
Alisema Zakaria alipiga kelele akimwita kwa jina lake ili akamsaidie.

“Nilikimbilia eneo la tukio nikasikia sauti ya mpige risasi huyo. Hapo ndipo nikasikia milio ya risasi na ghafla nikawa nimeshakamatwa na kulazwa chini na watu hao,” alisema Athumani.

Alisema kuwasili kwa basi la kampuni ya Zakaria kutoka Mwanza kuliwaokoa kwa kuwa abiria, wafanyakazi na wananchi wengine wakiwamo waendesha pikipiki walikwenda kutoa msaada.[/B]

Samuel Chomete (65), msemaji wa familia alisema tukio hilo limeibua hofu kuhusu usalama na uhai wa Zakaria kutokana na jinsi lilivyotokea na taarifa zilizotolewa na viongozi na mamlaka za Serikali.

“Hatujui lengo la waliojaribu kumteka mdogo wangu Zakaria, lakini tunaamini hawakuwa na nia njema ndiyo maana walifika usiku bila taarifa kama wanaokwenda kukamata jambazi,” alisema Chomete.

Alisema licha ya kuwa mfanyabiashara maarufu na kada wa CCM, Zakaria pia ni mfadhili wa masuala mbalimbali ya chama na kijamii ambaye angeweza kuitwa na kwenda mwenyewe Polisi iwapo alihitajika kwa jambo lolote.

“Tunamshukuru Mungu aliweza kupambana na watu kujitokeza kumsaidia. Pengine naye angepotea kama wengine wanaoripotiwa kupotea katika siku za hivi karibuni,” alisema.

Alisema, “Tumeiachia Serikali usalama na maisha ya Zakaria, akidhurika hata kidole familia tutaelekeza lawama zote dhidi ya Serikali kwa sababu imethibitika wahusika ni watumishi wa Serikali.”

Akizungumza na Mwananchi jana, mkuu wa mkoa wa Mara, Malima alisisitiza usahihi wa taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi akisema iwapo walioshuhudia wana kauli na maelezo kinzani, ukweli utajulikana suala hilo likifikishwa mahakamani.

“Nisikilize kwa makini, mimi ndiye mkuu wa mkoa, nimetoa taarifa juzi kwa waandishi wa habari na mwakilishi wa Mwananchi alikuwapo. Kama familia na mashuhuda wanasema tofauti mimi siwezi kusema lolote. Tusubiri suala hilo lifike mahakamani na yote yatajulikana huko,” alisema.

Malima alisema, “Siwezi kusema hivi jana halafu kesho niseme vingine na keshokutwa niseme tofauti. Mwananchi ni chombo makini mtaamua namna ya kushughulika na kauli kinzani mnayopata kutoka kwa mashuhuda na familia.”

Juzi akizungumzia tukio hilo mjini Musoma, Malima alikanusha taarifa zilizodai Zakaria alikuwa ametekwa akisema alikamatwa na maofisa usalama waliomdhibiti baada ya yeye kuwajeruhi kwa risasi wenzao wawili walioshuka kwenye gari walipofika kujaza mafuta kwenye kituo chake mjini Tarime.

Fedha zatoweka

Chomete aliyesema alionana na Zakaria muda mfupi kabla ya kuzungumza na Mwananchi, alisema familia haijui ziliko Sh16.3 milioni alizokuwa nazo Zakaria kwenye mkoba muda mfupi kabla ya kukamatwa.

Mwenyekiti wa mtaa wa Starehe mjini Tarime kilipo kituo cha mafuta tukio lilikotokea, Bashiri Selemani alisema,

“Kwa siku tatu mfululizo nililishuhudia gari lililohusika katika tukio likiwa limeegeshwa nyuma ya kituo cha mafuta cha Zakaria wakijifanya kulifanyia matengenezo, hii inaonyesha walikuwa kwenye mtego kufuatilia nyendo za Zakaria.”

Selemani pia ni diwani wa Nyamisangura na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Tarime.

Seikali ya wapuuzi

Serikali ya wauaji, watu wasiojulikana wameumbuka.

Hatimae wasiojulikana wamejulikana.

Mwenyezi Mungu mkubwa Mkuu.

Mkuu wa Mkoa ameongea vizuri kwamba kama taarifa yake inakinzana na vyanzo vingine basi yeye hana la kuongeza. The thing ni kwamba alikosea tangu mwanzo pale alipojitokeza kuwa msemaji wa Jeshi la Polisi badala ya RPC kwenye jambo la mtu mmoja lenye dalili zote za jinai. Tulizoea kuona ma-RC wakisemea masuala ya ulinzi na usalama yanayogusa jamii kwa ujumla. Kwa mwenendo huu ni rahisi viongozi kutumika vibaya na kupoteza credibility mbele ya umma.

Jiwe anazidi kuvuliwa nguo lakini alivyo na upumbavu atajifanya hahusiki.

Umeandika vizuri sana Mkuu na hii Serikali jinsi inavyoamua kukaa kimya kwenye masuala mbali mbali muhimu nchini ikiwemo hili la Watanzania wengi kuishi huku wakiwa na taharuki kubwa kutokana na hali ya usalama wa raia nchini kuwa tete tusitegemee kusikia chochote kingine kutoka kwa Mkuu wa polisi mkoani na walio juu yake ikiwemo Waziri mpya wa mambo ya ndani. Watu wasiojulikana wameumbuka na si ajabu hawana uhusiano wowote na usalama wa Taifa.

Mkuu wa mkoa anaongea uongo kuwatetea watekaji ili kulinda ulaji wake, amuulize nchemba jinsi ambavyo uhalifu haulipi na pia hao anaowatumikia kuna siku watamgeuka baada ya kumtumia kama condom

Tunaongozwa na mataahira, nimelisikia tena taahira moja likiagiza watu eti wakaendeleze ukali huko walikopelekwa ili mambo yaende! Hovyo kabisa linaamini mtu akisimamia mambo kwa ukali ndio kutakuwana mafanikio, mamanina! Zakaria naye sijui kwa nini hana shabaha namna hiyo!!

Haiwezekani afuatilie bila sababu…

Kuna kitu atakua kafanya au wamefanyiana…

Cc: @Mahondaw

Mambo ya ajabu saaana. Duu we acha tuu. Sijui mwisho wake ni nini.

Serikali ya watekaji

Huku KT ni pa muhimu sana kupambana na mizengwe ya JF ya nyumbani.
Mod wakifuta uzi unauleta huku.

wasojulikana.

Ukimbizini rahaa,hatupangiwi cha kuandika.
Wasiojulikana aibu yao.najua na huku mpoo,dawa yenu ni tarime tuu

Ndo maana savimbi kafutwa kazi maana alikosea timing ya kumuua huyu. Na ukatili wote alionao savimbi sijui ni nini kilitokea misheni ilafeli ila Mungu ni mwema

shida ukikaa kimya unaonekana hufanyi kazi

Sijui kwa nini Zacharia hakuwamaliza kabisa.

ipo siku!.. nasema ipo siku.