Mapishi ya mkate wa kumimina


Mahitaji:

  1. Mchele nusu kilo
  2. Sukari robo kilo
  3. Hamira kijiko kimoja kidogo
  4. Hiliki ya kusaga nusu kijiko kikubwa
  5. Nazi mbili au tatu

Jinsi ya Kupika:

Chambua mchele na kutoa mawe, kisha loweka mchele huo kwa masaa manne (4).
Kuna nazi na uichuje tui zito vikombe vitatu (3) na tui linalobaki weka kwenye bakuli.
Chukua mchele weka kwenye blenda, weka sukari, hamira na hiliki na tui zito kijiko kimoja kisha saga.

Iwapo mchanganyika utakuwa mzito hadi blenda ishindwe kusaga vizuri, ongeza kidogo tui lile uliloacha kwenye bakuli kisha saga mpaka ulainike kabisa. Mimina kwenye sufuria safi na uache uumuke. Ukisha umuka weka sufuria kwenye moto, chukua tui zito kikombe kingine kimoja na umimine nusu kwenye sufuria usambaze kwenye sufuria ili ukiweka unga uliousaga usipate taabu ya kuutoa mkate kwenye sufuria utakapoiva.

Hakikisha hilo tui uliloweka chini ya sufuria linaiva na kuwa na rangi ya kahawia (brown) kisha mimina mchanganyiko wako uliosaga na usubiri kwa dakika 4. Weka mchanganyiko wako kwenye oven na baada ya muda funua kuangalia kama mkate utakuwa umeiva, chukua kisu cha mezani au uma na ubonyeze mkate katikati, kama hakuna dalili za majimaji basi mkate utakuwa umeiva. Chukua tena tui zito lililobaki na umimine kiasi huku unasambaza katika mkate wote na urudishe ndani ya oven kwa dakika chache na uutoe.

Chukua chombo chenye maji na kalisha sufuria ndani yake ili ipoe na uweze kuutoa mkate kwa urahisi, baada ya hapo mkate utakuwa tayari kwa kuliwa.
[ATTACH=full]180044[/ATTACH]

Waaow yummy

Sky Eclat, wewe ni mtaalamu wa mapishi au mchambuzi, maana unaonekana fundi pande hiziā€¦

Kwenye uchomaji hapo

Hua napendelea zaidi kwneye mkaa na hua nafajya hivi

Nahakikisha sufuria imekaa sawa moto chini wa wastan namimina mafuta yakishapata moto nachanganya unga wangu nilosaga halaf naacha vikae kidogo then naweka mfuniko juu wa moto mkate upande
Kujua umeivahua nakua na kijiti natengeneza chelewa ile naikwangua na kisu naosha then natoboa kuona wapi panahitaj moto au kupunguza na kuiva kabisa

Shukran

Karibu

Yummy