Vipimo
Maharage - 3 Vikombe
Tui la nazi zito - 1½ kikombe
Kitunguu - 1 kikubwa
Nyanya - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi - 3
Chumvi - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
[ol]
[li] Chemsha maharage hadi yawive haswa yalainike [/li][li]Katakata kitunguu, nyanya, na thomu kisha miminia katika maharage [/li][li]Tia tui la nazi na subiri kidogo lichemkie humo [/li][li]Weka chumvi kiasi na koroga iliuonje, kisha tupia pilipili mbichi na kisha funika kwa muda kadhaa hadi libaki rojo rojo [/li][li]Baada ya hapo pakua na tayari kuliwa[/li][/ol]
[ATTACH=full]180046[/ATTACH]