[FONT=courier new]Leo katika pita pita yangu maeneo fulani hivi ambako ni Hospitalini nilishikwa na ’ butwaa ’ lakini kwa ’ vituko ’ vichache nilivyoviona ilinibidi tu leo ’ mbavu ’ zangu ziwe na Kazi ya ziada kwa Kucheka jinsi Wahudumu wawili wa Chumba cha Maiti ( Mortuary Attendants ) walivyokuwa wanafanya.
Kituko # 1.
Imefika Saa Saba ( 7 ) za mchana walikuwa wamekaa nje ya Chumba chao cha Maiti huku wakiwa wamelala / wamejipumzisha mara ghafla wakawa wanamlaumu Nesi wa zamu leo kwa kuwanyima ’ ulaji ’ wakimaanisha kwamba imekuwaje hadi muda huo wa Saa Saba ( 7 ) hajawapigia Simu waende ’ Wodini ’ kubeba Maiti ili waje kuziosha na wajipatie Fedha?
Kituko # 2.
Mida ya kama Saa Kumi ( 10 ) hivi za Jioni eneo hilo hilo nikawasikia tena wakilalamika kwamba ’ Maiti ’ zimejazana hovyo na zinawanyima wao ’ Ulaji ’ kwani Watu wengine watashindwa kuwaleta hapo Ndugu, Jamaa na Marafiki zao huku ’ Nyuso ’ zao zikiwa zimenuna / zimekasirika kabisa.
Kituko # 3.
Huyu Mhudumu nadhani kama ni Bange / Bangi ambayo anaivuta basi nadhani hata Muasisi wake Hayati Bob Marley hakuwahi kuigundua na kama Wahusika wa hiyo Hospitali hawatokuwa makini nae kuna Siku atakuja kufanya ’ Kitu ’ cha ajabu mno hapo. Mida ya Saa Kumi na Mbili ( 12 ) jioni wakati Watu wanatoka kuwaona Wagonjwa wao katika hali isiyo ya kawaida huyu Mhudumu wa Chumba cha Maiti aliingia katika ’ Wodi ’ moja kisha akawa anauliza namnukuu…" Hivi nyie leo hamfi tu? Sasa mnadhani msipokufa Sisi tutapaje Mishahara yetu? Hebu kufeni bhana!.." kisha akatoka na kwenda katika Wodi zingine. Nilijaribu kudadisi kidogo kwa Watu waliomzoea pale na jibu nililopewa ni fupi tu na nyoofu kwamba huyo ukimuhoji tu tegemea ’ matusi ’ ambayo pengine tokea uzaliwe hujawahi kuyasikia na ukifanya mzaha unaweza ukapigwa ’ Ngumi ’ ambayo hata Floyd Myweither hajawahi na hajafikiria kuipiga bado.
Naomba kujua hawa Wahudumu wa Vyumba vya Maiti wana ’ akili ’ timamu hizi hizi kama zetu au?
Nawasilisha.[/FONT]