Kwa wapenzi wa korea drama hii ndiyo thread yako

Yule jamaa nilimkubali sana alipocheza series ya punch Na empress ki. Ila aliniboa sana kwenye frozen flower

Hivi frozen flower ndio aliigiza gay? Ila ni kutimiza majukumu tu hahaaaaa

Ndiyo hiyo hiyo

daebak muandiko wako nishauhifadhi.
a poem a day niliishia njiani baada ya kuona baadhi ya characters wana tabia za kitoto kama za kiongozi wa nchi fulani iliopo Afrika.
nilivutiwa zaidi na mashairi yaliokuwa yakisimuliwa.

Hahahaha njoo uzi wa kupeana likes au kule sports utanifahamu tu.

Imeisha vizuri mkuu. Nimezipenda tabia zao hivyo hivyo.

aigooooo
huwezi kuamini tokea JF isitishe kutoa huduma zake sijawahi kukosa kutembelea kenya talk, niliamini JF itarudi baada ya siku chache lakini cha kushangaza wiki ya pili inamalizika na sioni dalili ya JF kurudi hewani na ndio maana leo nimejisajili ,cha kushangaza nimejikuta nikirudishwa kwenye utawala wa joseon (NEW VILLAGE).

하하하 하하 하하하 하하
unataka kunifanya niirudie tena, kuna daktari mmoja alikuwa na tabia za ajabu kweli na aliniacha na maswali mengi yasio na majibu.
alikuwa hawezi kufanya jambo bila ya kujiuliza maswali mara 10.
nifanye au nisifanye
nivae nguo hii au nisivae
kama nikivaa itakuwajie,kama nisipovaa je itakuwajie.

mwanzo nilikuwa nachukia mpaka mwisho nikamzoea vituko vyake

Hahahaa kwa kesi ya huyo inahitaji uvumilivu mkubwa ila uzuri wenzie kazin walimzoea fasta hasa yule kijana msaidizi wake.
Nilimpenda yule mwenye swaga za May i give u advice

huu muandiko kama wa shaibu hiwalisi a.k.a wang guhn.
acha tu huyo kim joo hyuk ahjussi aendelee kupumzika kwa amani kwenye nyumba yake ya milele.
miezi 8 imetimia tokea afariki dunia
[ATTACH=full]178780[/ATTACH]

JF ilikua inarudi kwa njia nyingine sema tcra wakaharibu mpango kwa kuongeza siku za kujisajili toka june 15 mpaka june 30 hivyo tutegemee JF kurudi mwezi wa saba

하하하 하하 하하하 하하
wafanyakazi wenzake walikuwa wanamkimbia ila bwanamdogo aliona isiwe tabu kama anajifanya mwehu na mimi nizaidi ya mwehu.
hivi lee joon hyuk a.k.a mzee wa kutoa ushauri ndiye lead actor?
nimemkumbuka kwenye city hunter na harakati zake za kumtafuta Lee Yun-Seong.
halafu kwenye drama mpya ya are you human pia yumo.
[ATTACH=full]178782[/ATTACH]

Aigoooooo
Nafurahi kukuona hapa Mkuu.

siku 11 bila ya JF
miezi 11 bila ya kusoma comment yako
daebak, huu wimbo umemaliza maneno yote niliotaka kuandika.
bogoshipo noona

https://www.youtube.com/watch?v=kR1XfuVeZTY

Yule jamaa alimvumilia sana. Akaja ibuka mr decisive yaan yeye akiamua kaamua wakalazwa wodi moja basi vurugu tupu hahaha, indecisive vs decisive

Lee ndio stering huyu yupo vizuri kweli.

Are you human too naisubiria iishe maana masuala ya kufuatilia ongoing ni kujitafutia headache tu,kuna ongoing(my golden life) ilinitesa nikaapa sitarudia ugonjwa huu

What a coincidence?
Niliwakosea kweli wapenzi wangu,mimi nilikuwa nawasoma kila nipatapo nafasi… ila nimerejea sasa.
I won’t leave you guys.

hili kombe la dunia nalo limeleta balaa mpaka korea.
drama nyingi zinazoonyeshwa na mashirika ya umma hazijaendelea wiki hii.
wok of love
are you human
partners for justice
come and hug me

cable tv hawana muda wa kombe la dunia ni mwendo wa drama mpaka unazikimbia

aigoooo itabidi nile matapishi yangu.
a poem a day drama nilifika episode ya 6 nikaachana nayo.
si unajua hizi drama hatujibii mtihani wa fasihi sasa balaa unakuta mtu anataka kuangalia drama zote za wakorea zinazoonyeshwa na zilizoonyeshwa.
siwezi kumsahau mchangiaji mmoja kwenye JF aliposema ameangalia drama zote za korea

Kombe ni balaa kila kona hapo sasa watu kuendelea na viporo ni mpaka july kombe likifika ukingoni

Hahahaha huyo sio mkweli duh korea ina drama nyingi sana mtu hawezi maliza zote.
Ipo vizuri hutaijutia na nyimbo zao tamu ila wakorea walevi jaman hasa soju lakin hawalewi mpaka kupoteza network sijui ni maigizo tu au hata maisha halisi

gwenchanah gwenchanah.
[ATTACH=full]178797[/ATTACH]
anakusalimia choi min soo ahjussi
balaa lake si dogo kwenye drama ya lawless lawyer
amekutana na lee joon gi ni shidaaa
lafudhi yake ya kikorea ndio hunimaliza zaidi anapozungumza
bong sang piliiiiiiiiiiiiiii ujuweeeee kamaaa niliweza kumuua mama yakoooo na mjomba wakooooo basiii hata wewe nitakumalizaaaaaaaa
하하하 하하하하하 하하

annyeonghi jumuseyo = usiku mwema