[FONT=courier new]Sitaki kuvitaja hapa Vyuo husika ila kwa vingi ambavyo nimevipitia hapa Jijini Dar es Salaam nimegundua ya kwamba 95% ya Wanafunzi wake wa Bachelor Degree na Masters Degree researches / dissertations zao wanafanyiwa na Watu ’ Maalum ’ kwa malipo ’ Maalum ’ kisha muda ukifika Wao wanazifuata tu na kwenda kuzifanyia ’ defending ’ katika ’ Panels ’ husika wakimaliza wanakuja ’ Kutamba ’ mitaani kuwa wameelimika na wao ni Wasomi wa Kutukuka.
Tusijidanganye kwa sasa Tanzania hatuna tena ’ Typical Intellectuals ’ bali tuna ’ Fake Intellectuals '. Nimekasirika na kuchukia mno hasa baada ya jana tu nikiwa maeneo ya Sinza kuwaona Vijana fulani wa Vyuo Vikuu vya hapa Jijini Dar es Salaam baadhi wakiwa ’ wanabeti ’ na wengine wakiwa ’ wanagambeka ’ halafu wanawapigia Simu Watu wanaowafanyia na kuwaandikia hizo researches / dissertations zao kama ziko tayari au bado ili wapate Vyeti vyao na wajiite Wasomi.
Acheni tu Wakenya, Waganda na Wanyarwanda watushinde Kielimu na watuache Kimaendeleo hakyanani!
Nawasilisha.[/FONT]