kwa katiba ya tanzania hata kitoto kichanga kinaweza kuongoza nchi

kwa mambo yalivyo sasa hata kitoto kidogo cha miaka 2 kinaweza kuongoza taifa smoothly,silent and quietly ,kunahaja ya kuhoji uzalendo wa mtu aliyeandika katiba ya jamhuri ya muungano kama kweli anachembe ya damu ya kizalendo kwa taifa, inawezekana katiba ya tanzania haikuandikwa na mtanzania bali iliandikwa na wavamizi wenye sura ya kitanzani waliotaka kuchuma mali za taifa letu na kujifanya kuwa ni wazalendo,hivi kwa katiba yetu ambaye mtawala anaweza akafanya lolote la kusaidia wananchi ama kuwaangamiza na hakuna anaweza kuhoji lolote linalo amuliwa na watawala basi kitoto kidogo cha miaka 2 kinaweza kikaongoza tanzania bila shida ,katiba itakilinda kikiamua lolote hakuna wakuhoji,
kikiamua kununua pipi kwa kodi za wananchi na kutoa hoja kwamba pipi hizo zitasaidia watoto wenye uhitaji wa pipi -hakuna atakaye hoji
kikiamua kununu mapulizo kwa kodi za wananchi na kuyasambaza nchi nzima na kudai kuwa yatapendezesha nchi na kuwavutia watoto wa kizungu kuja kutalii -hakuna awezae kuhoji
kikinamua kununu midoli kwa kodi za wananchi na kuwagawia watoto wote nchi nzima na kudai kuwa ni upendo kwa watoto -hakuna wakuweza kuhoji
cry for tanzania

Hakika

Njia ya kuzuia hayo yasitokee ipo… ila hakuna aliyetayari kumwagia kitumbua chake mchanga…

Kila mtu anafunika kombe ili mwanaharamu apite…

Cc: @Mahondaw