Kwa hatua hizi tayali tumesharudishwa kwenye UJAMAA hivyo tuupinge kwa nguvu zote

Hakuna asiyejua definition ya Ujamaa(umaskini) -
Ujamaa ni mfumo wa kimaskini yaani ujima, mfumo wa kugawana umaskini,ni mfumo ambao haukufikirishi ili uishi.

Hivi sasa naona tunarudishwa kwenye ujima ambao tulishakuwa tunauacha baada ya kuona hauna tija na ukabakia kwenye Katiba tu. Na nchi nyingi zilizokuwa zinaufuata zikaamua kuachana nao na kufuata mifumo ya kati ya kibepari.

Na hizi ni hatua tayali tumeshafika za kurudishwa kwenye Ujamaa,

Tunahimizwa lazima tuwe na kipato sawa, hapa kiuhalisia haiwezekani hata ndani ya familia hili ngumu , mmoja kuonekana kupendwa na wazazi ni kawaida.

Kujitokeza kwa vikundi vya kuaminisha wengine kuwa huyu ndiye anaweza kuongoza na mwingine hapana. Wengine wanatakiwa kumsikiliza mmoja tu kwa kuwa ndiye tumemchagua wala asionekane wa kupinga.

Kwenye Ujamaa ili ufanikiwe mabavu lazima yatumike sana ili kupunguza ukosoaji au hutengenezwa mfumo mmoja wa uwasilishaji wa mawazo.(hayo tunayaona kupunguzwa kwa nguvu ya mitandao ya kijamii)
Kwani ukiruhusu mawazo mengi na uhuru wa mitazamo tofauti Ujamaa hauwezi kufanikiwa.

Kwenye Ujamaa MAKATAZO NI MENGI KULIKO KUJIFUNZA MAPYA( there are so many dont’s than do’s) Sheria na kanuni zinasisitizwa zaidi kuliko mawazo mbadala hivyo huvunja ubunifu kulinganisha na ubepari. Tunaona jinsi Sheria zinavyoongezwa na kusisitizwa Tusivunje Amani.

Kuanza kuwaona matajiri ni wezi/majizi yametuibia , utajiri wao umetokana na kutuibia na utajiri ni kama dhambi umaskini ni kama sifa kubwa ndio maana tunaona mtu anajisifu kuwa mimi ni Kiongozi wa masikini.

Kuchukia Sekta binafsi(tunaona yaliyotokea kwa FastJet kunyang’anywa ruti na kupewa ATCL.

Kuimba nyimbo za kutukuza na uzalendo (hapa tunaona TBC na vipindi vyake) usipoimba wewe ni Kibaraka.

Na mengi ambayo yanaonesha dhahili tunarudishwa kwenye Ujamaa.

KWANINI TUUPINGE?

Mfumo wa elimu unaotawala dunia ni wa kibepari hivyo masomo yenyewe, mitaala ya elimu kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu ni ya kibepari na si ya kijamaa.

kuona matajir wez,kuimba nyimbo za kumsifu hiz zinakera mno tena sana! aondoke tu.

Magufool kwenye ubora wake wa upumbavu.

Jitu likitokea kwenye umaskini sana linakuwa lina roho mbaya sana

Mkuu usipotoshemaana ya ujamaa, hayo yote uliyo ya taja sio ujamaa, ni udhalimu wa uongozi na chama kinacho tawala. Tabia mienendo au hulka za vingozi si falsafa za ki uchumi. Ujamam unaweza kuutafsiri kma “a political and economic theory of social organization which advocates that the means of production, distribution, and exchange should be owned or regulated by the community as a whole.” Sas hapo ndugu yangu kwa neno community si serekali bali ni wananchi kupitia vyama vyao vya ushirika au kwa namna inayolingana na hivyo. Hebu angalia baadhi ya nchi ambazo ni za kijamaa duniani ni kama ,Denmark, Finland, Netherlands, Canada, Sweden, Norway, Ireland, New Zealand, Belgium kwa uchae tu, je zina huo udhalimu. Mkuu usitafute kisingizio kwenye mfumo wa kiuchumi ambao haupo na chma tawala kiliisha utupa pembeni.

I have a reservation on your post. I fully support your definition of socialism but opposes your assertion that all the countries you listed are socialist. Example Denmark follows highly developed mixed economy, sio ujamaa wa kipuuzi wa akina Fidel, Julius na Tito ambao ulikuwa unapandikiza ujinga kwenye vichwa vya watu.

Hili la kumuona tajiri ni mwizi ndio umasikini kiwango cha lami kabisa.

Ujamaa haufanyi watu kufikiri bali tunakaa na kusubiri nani wa kututatulia matatizo

Sidhani kama ni sahihi kusema kuwa kuna ujamaa wa Fidel, Julius au Tito, falsafa ya uchumi wa kijamaa ni universal, jaribu kutenganisha falsafa na mtindo wa uongozi wa nchi. Pricipals za ujamaa zikiwa applied vizuri na sahihi nchi ambayo masikini isiyoweza kumudu maendeleo chini ya mfumo wa ubepari huweza kupata maendeleo kwa haraka sana. Hivyo mkuu ujamaa kama falsafa haina mataizo, matatizo ni watawala.

Urusi na China walikwisha achana na mfumu huu na sasa ona wanavyopiga hatua za maendeleo!! Cuba peke yake bado inang’ang’ania mfumo huu na wananchi wake wako katika mateso makubwa!!

Maendeleo ya Urusi na China yaliweza kupiga hatua kubwa mno chini ya mfumo wa kikoministi haukuwa wa kijmaa. Maendeleo unayo yaona leo kwa nchi hizo chanzo chake ni mfumo huo wa awali. Ukiangalia historia ya China ilikuwa ni nchi masikini, lakini kwa kipindi kifupi sana chini ya falsafa yao ya kikoministi walipata maendeleo makubwa sana. Cuba ni ka nchi kadogo sana na ilikuwa nchi ya dunia ya tatu, lakini chini ya mfumo wa kijamaa wamepata maendeleo makubwa sana. Mkuu niambie uchumi wa Cuba unaweza kuulinganisha na nchi ipi Africa?

Kwa sasa hakuna nchi inayofuata ujamaa ikapiga hatua kimaendeleo, ujamaa hauruhusu unyonyaji na katika dunia ya leo huwezi kuendelea pasipo unyonyaji

Mpe somo huyo

Acha kuunga unga stori na kutudanganya rudi darasani ukasome zaidi maana ya ujamaa

Kwahiyo watanzania wasifanye makossa tena,chaguzi zijazo wajue nani wakumchagua ili wawaongoze,sio kila mtu ana uwezo wa kuwaongoza wenzake,duniani kuna watu wa aina mbili waongozaji “leaders” na wanaoongozwaji “followers”…

Magufuli sio mtu mbaya lakini hana uwezo wa kuongoza wenzake,Yeye mwenyewe analijua hilo,na ndio maana alichukua fomu ya kugombania uraisi mwisho kabisa baada ya kulazimishwa,…

Marehemu Kingunge aliwahi kusema kuwa Magufuli mwisho wake ni kuwa mnyapala wa kutengeneza barabara…
Watanzania imefika wakati tuache ushabiki wa vyama,watanzania tunakiwa tuangalia nani anaweza kutuongoza,bila ya kuangalia anaetuongoza anatokea chama gani cha siasa…

Wafuasi wa jiwe utawafahamu tu.

Ebu weka elimu yako hapa yenye kutafsiri misingi ya ujamaa

Nakuona akili yako imekaa kiulemavu lemavu sana kiasi cha kushangilia kila jambo kishabiki pasipo kuweka fact zako hapa zenye kupinga kwa hoja thread ya mleta mada

Kinyago mmekichonga wenyewe sasa chawatisha hadi mlokichonga…!!!