Shabash! Ni juma lingine jipya ambalo mola ametujalia kuweza kuwa pamoja na kuifanikisha hino fani kwenye hichi kijiji chetu. Leo tutapambanua misamiati ambayo huwa tunakumbana nayo katika usemi wetu wa kila siku na kwa mara nyingi huwa ni kwa lugha ya kiingereza. Tujaribu kutafuta tafsiri yake katika lugha ya Kiswahili.
Karibuni.
Baadhi ya hayo maneno ni kama;
-Scatterbrain …Mapepe
-Abject………dhila
-Abjectness…udhalifu/udhilifu
-Masters Degree…Shahada ya Uzamili
-PhD…Shahada ya Uzamifu
-Abstain…Kujihimili
-Abolition…kitanguo/ukomeshaji/uvunjo/uvunjaji/uvunjifu
ZOEZI
Kwa Kiswahili sanifu tafsiri maneno yafuatayo.
-Thesis…
-Taboo…
-Scan…
-Headscarf (worn by women)…
-Accord…
-Accountancy…
-Acne…
-Scalpel…
-Aroma…
-Abyss (like in a gorge)…
-Abortion…