[SPOILER=“WARNING: DISTURBING IMAGES”] [ATTACH=full]88397[/ATTACH] [ATTACH=full]88396[/ATTACH] [ATTACH=full]88395[/ATTACH]
[ATTACH=full]88398[/ATTACH]
[/SPOILER]
Kaswende ( ing. syphilis ) ni mojawapo kati ya maradhi ya zinaa ambayo inasababishwa na bakteria inayofahamika kama Treponema pallidum .
Katika hatua za mwanzo, vipele katika sehemu za uzazi huanza kujitokeza muda mfupi baada ya maambukizi ambavyo baadaye hupotea vyenyewe.
Kama ugonjwa hautatibiwa,
maambukizi huendelea kwa miaka, yakishambulia mifupa , ubongo na moyo na kusababisha madhara mengine yanayotokana na matatizo katika mfumo wa fahamu kama vile homa ya uti wa mgongo na magonjwa ya moyo na kiharusi .
Kaswende wakati wa ujauzito
unaweza kuwa hatari kubwa kwa
kiumbe tumboni, kama vile
kusababisha kutoumbika vizuri
( deformity ) na kifo .
Wanawake wengi wajawazito katika nchi zilizoendelea huchunguzwa kwa uwepo wa ugonjwa huu katika majuma ya kwanza ya mimba ili kutibu ugonjwa kabla kitoto
hakijaathirika.
Siku hizi kaswende inaweza kutibika kwa urahisi fulani kwa penicillin .