Kadrinali Pengo Anaondoka au Anang'olewa

Kumekuwa na taarifa za kuteuliwa kwa Askofu mpya Mkuu mwandamizi kwa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, kama ni hivyo nafasi ya Kadrinali Pengo iko wapi, je anajiuzulu au anaondolewa?

Hivi ukiwa kazini halafu unakwenda kununua gazeti na unakuta nafasi yako inatangazwa unafanyaje vile?

Vatican huwa hawapendi kabisa ujinga!!

Muda wa Kustaafu umefika

Itakua anaondolewa

Hii mutu Pengo ikistaafu itaafaa iitwe “Mjinga aliyezeeka” Not Mzee.

pengo ana kila sababu ya kujiuliza ni kwa nn watu wanafurahia sana taarifa hizi, hili si jambo jema kwa kiongozi wa kidini

alikua kikwazo kwa maaskofu wenzake, utengano haufai kwenye kanisa lazima wote wawe na kauli moja

akapumzike tu maana hakuna namna

duuuh! hii kali mkuu

Cardinal Pengo lazima aondoke haikuwepo njia nyingine zaidi ya kuondolewa.

Mosi Waraka uliotolewa na Kanisa Catholic ni sababu kubwa na toshelezi ya kumweka kando Cardinal Pengo.
a. Utaratibu wa kanisa Catholic kabla ya kutoa Waraka lazima upitie stages mbali mbali na mwisho Waraka unasajiliwa Vatican hivyo kuufanya Waraka mali ya kanisa.

b. Hivyo inspotokea Askofu mmoja anakwenda kinyume na maazimio ya Waraka maana yake anapingana na Vatican ambao wameusajili waraka na kuufanya mali ya kanisa.

c. Ilikuwa suala la muda tu kabla Cardinal Pengo hajatupwa na Kanisa kwasababu kwa muda mrefu alikuwa akienda kinyume na maazimio ya Baraza la maAskofu.Kwa hakika kama si busara za maAskofu tungeshuhudia kauli za ajabu za kuzalilisha kanisa.

d. Kwa hakika haki,utu,busara na heshima ya kanisa zilidumishwa na kuhifaziwa kipindi chote ambacho Cardinal Pengo aliyatazama maslahi ya serekali dhidi ya maslahi ya haki,utu,heshima na uhuru wa waTanzania.

e. Kanisa Catholic Tanzania litasimama kwakuwa limesimama katika haki.
KKKT litasimama kwasababu limesimama katika haki.Wakuu wa makanisa haya Kwa hakika historia itaeapatia nafasi kubwa si kwasababu ya ukubwa wa makanisa yao bali kwasababu ya kile wanachokisimamia.

Mungu ibaraki KKKT ,Mungu ibaraki Kanisa Catholic Tanzania .

Kama ni kung’olewa itapendeza zaidi…

Yale maharage aliyokula sasa yamejulikana ni maharage gani na ya wapi