Jumla ya watu 641 wamefikishwa Mahakamani kwa makosa ya Uhaini, Unyang'anyi wa kutumia Silaha kutokana na maandamano na vurugu zilizotokea nchini kuanzia Oktoba 29

umla ya watu 641 wamefikishwa Mahakamani hadi sasa wakishtakiwa kwa makosa ya uhaini na makosa mengine yanayohusishwa moja kwa moja na maandamano na vurugu zilizotokea nchini kuanzia Oktoba 29 mwaka huu

Mawakili Maduhu Williams, Paul Kisabo na Dickson Matata wamezungumza na Wanahabari leo, Jumanne Novemba 11.2025 kama wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na miongoni mwa Mawakili walioteuliwa na chama hicho kuhakikisha wanatoa msaada wa kisheria bila malipo kwa washtakiwa hao walioko maeneo mbalimbali nchini, sambamba na wale ambao bado wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi

Katika maelezo yao wamesema, miongoni mwa washtakiwa hao 240 wako Dar es Salaam wakishtakiwa kwa makosa ya uhaini, Mwanza 172 wakishtakiwa kwa unyang’anyi wa kutumia silaha, uchomaji mali, uharibifu wa mali na kufanya vurugu, Dodoma wapo washtakiwa 32 wakishtakiwa na uhaini, na Kigoma wapo 11 wanaoshikiliwa kwa unyang’anyi wa kutumia silaha

Kwingineko Iringa wapo 89 wakishtakiwa kwa uhaini na unyang’anyi wa kutumia silaha, Njombe kuna washtakiwa wa uhaini tisa (9), Tabora kuna watano (5) wanaoendelea kushikiliwa Polisi, Bunda kuna 29, Tarime tisa (9) na Mafinga 45 wote wakishtakiwa kwa makosa ya uhaini

Wakati huohuo, Mawakili hao wamesema bado hadi sasa hawajapata hati ya mashtaka inayowahusu washtakiwa wa Arusha ambao wamefikishwa Mahakamani kwma makosa ya uhaini

“Kutokana na makosa mengi yanayowakabili watuhumiwa kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria, baada ya mashtaka yao kusomwa Mahakamani, kwa Dar es Salaam watuhumiwa walipelekwa katika gerezani la Segerea” -Mawakili

Mawakili hao wamewaeleza Wanahabari kuwa, adhabu ya juu kabisa wanayoweza kukutana wateja wao endapo watakutwa na hatia ni kunyongwa hadi kufa, huku adhabu inayofuata ikiwa ni kifungo cha maisha jela, huku adhabu ya chini ikiwa ni kifungo cha miaka 30 jela, hivyo kutokana na uzito wa adhabu hizo chini ya mwavuli wa TLS Mawakili hao wameahidi kutoa ya utetezi inayostahili na kwa ukamilifu wake kisheria…

https://www.instagram.com/p/DQ6ntQlAqdR/?hl=en

Askofu mkuu wa katoliki Tanzania amkemea vikali Suluhu kwa kuwaua watu wengi sana

Kwikwikwikwikwi Kundudweller mnapotosha sana jamii. Mnaiogopa sana Tanzania mpaka mnaeneza taarifa za uongo everyday

Idi Amin Mama apelekwe ICC we cannot condone dictators at our doorstep

Mwalimu Nyerere aliwawuon nyinyi CCM… mumekuwa chama cha matajiri