Jukwaa la Afrika mashariki.

Nawasalim wanakijiji wote hapa jamvini. Naomba sasa nijikite kwenye mada yangu.

Lengo la kuomba jukwaa la Afrika mashariki ambalo ndani yake linaweza kugawanywa katika nchi husika kuendana na uwingi wa watumiaji wake hapa, kunatokana na sababu zifuatazo!

1; Kuondoa mwingiliano wa mada zinazohusu nchi ya Kenya (ambapo ndipo jukwaa hili lilipo) na nchi nyingine au majukwaa mengine.

2; Kuwa na uharaka wa kupata mada za nchi husika hasa kwa watumiaji wanaotoka nchi hizo! Kwa hali ilivyo sasa hivi tunatumia mda mrefu kupata mada za nchi nyingine pale ambapo lengo letu linakuwa ni hilo.

Hatua hii mbali na mambo mengine itaongeza idadi ya watumiaji wa jukwaa hili lakini pia idadi ya mada zitakazokuwa zinajadiliwa itaongezeka.

Naamini wasimamizi mtalifanyia kazi ombi hili!

Naomba kuwasilisha

kuna seksheni ya News & Politics ama ukipenda Habari Na Siasa.

Naiona, lakini iko too general.