Nadhan tunafaham vileja vikoje, ni jamii ya biscuits viko vya aina nyingi lakini leo ntaeleza namna ya kupika vileja navyojua mie
Mahitaji
Unga wa ngano kg 1
Mayai 4 hata 3 sio mbaya
Siagi nusu
Sukari itategemea unataka vya sjkari nyingi zaidi au kiasi
Baking powder
Namna ya kutayarisha
Chukua siagi na sukari mix kamavile wafanya kwenye keki changanya had uone sukari na siagi vimechanganyika kabisa
Weka baking powder kijiko kimoja cha chai usijaze sana
Changanya tena baking powder na mchanganyiko huo hapo juu
Vunjia mayai yako yite kwenye mkorogo wako then changanya had uone yai limejichanganya na siag na sukar yana kama vile kwenye keki
Mimina unga wako kidogo kidogo huku ukichanganya kwamkono kama vile unakanda unga
Hakikisha haviwi vigum sana wala lini sana viwe kati kwa kat
Tayarisha kibao chako cha chapat na mskumio na unga kidogo wa kushikia
NyunyiIa unga kwenye kibao chako wakat huo ule mchanganyiko wako umekata matonge tayar kwa kusukuma
Najua mtajiuliza why hapa vjnaoneaka kuna heart shape round shape hivo n vbat special kama huna tumia glass tu ya udongo ile
Hakikisha husukumi sana wala kuufanya mzito sana then zungushia glass kwenye unga wako uliosukuma kupata shape
Fanya hivo kwa matonge yaliyobakia
Chukua kiokeo chako hata sufuria pakaza mafuta panga vileja vyako
Vioke kwa mtoto mdogo mdogo had upate rang utakayo
Wabillah taufiq
@Madame S