JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA YA NG`OMBE

Karibu katika jiko na mapishi, na leo tutajifunza kupika pilau la nyama ya ngombe. VIPIMO, [ul] [li]Mchele 2kg[/li][li]Nyama ya ngombe 1k[/li][li]Pilpilihoho 1kubwa[/li][li]Nyanya 3kubwa[/li][li]Vitungu maji 2vikubwa[/li][li]Thomu iliyosagwa 1kimoja cha supu[/li][li]Tangawizi 1kijiko kimoji cha chai[/li][li]Mafuta ya kupikia 1/2 kikombe[/li][li]Binzari nyembamba 1kijiko kimoja cha chai[/li][li]Pilpili manga1/2 kijiko cha chai[/li][li]Hiliki 1/2 kijiko cha chai [/li][/ul]
JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA YA NG`OMBE
[ol]
[li]Loweka mchele wako katika chombo,[/li][li]Chukua nyama na uioshe na itie thomu,tangawizi,ndimu,pilipili manga, na chumvi kiasi[/li][li]Iweke jikoni hadi ikauke maji,na maji yakikauka ikaangekaange ka hayo hayo mafuta ambayo uliyaweka mwanzo hadi kuwa rangi ya hudhurungi(broun)[/li][li]Katakata vitunguu na nyanya pembeni[/li][li]Chukua pilpil manga,thomu,tangawizi na uvisage katika mashine ya kusagia au kinu,[/li][li]Weka sufuria jikoni na utie mafuta,subiri yapate moto,[/li][li]Kisha tia vitungu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya[/li][li]Kisha mimina mchanganyaiko wako ulio usaga na pilpil mang thomu na tangawizi,[/li][li]Koroga kwa dakika kathaa kisha mimina nyama iliyokuwa tayari maji kisha na chumvi kidogo nasubili maji yachemke na weka mchele wako uchanganye vizuri ili uchanganyike na viungo vyako pamoja na nyama isikae sehemu moja[/li][li]Funika hadi maji yakauke,na ugeuze kama umeiva kama bado ufunike tena,subili kw dakika chake, na hapo chakula chako kitakuwa tayali kwa kuliwa[/li][/ol]
[ATTACH=full]178337[/ATTACH]

Ahsante sana

[COLOR=rgb(251, 160, 38)]Nice

Babu Asprin anafaidi sana maakuli haya

Kesho ntafata procedure zote hizo ntoe kitu…karibun sana

[SIZE=5]Tatizo la mapishi ya mtandaoni yana list ndefu mno. mahitaji ishirini na zaidi.
ukute yeye mwenyewe akitaka kupika hana na haweki vyote hivyo.
nyie wanawake kina @Sky Eclat @NAHUJA @Evelyn Salt kwanini hamuwi realistic katika mapishi[/SIZE]

Ha ha ha acha uvivu bana andaa vitu upike kama hapo nini sio cha kweli?
Halafu mahitaji yanatofautiana mi naweza tumia viungo we ukaunguza tu vitunguu na wote tukawa tumepika pilau usijali kuhusu mahitaji.
Unaangalia unavyopenda wewe usivyovipenda unaviacha

Sky Eclat, heshima kwako! Ila tatizo la kusoma habari za mapishi wakati una njaa…

kesho ntajaribu kutoa pilau