Nianze kwa kuwapongeza Maxence Melo na team yake yote kwa kuweza kuirudisha hewani JF og kipenzi cha watanzania wengi watumiaji wa social media, hakika amefanya jambo zuri na kubwa zaidi.
Ila nimejaribu kuingia kama mgeni na kajaribu kupekua forum kadhaa kuangalia nini kinaendelea, tahamaki nimegundua JF imekuwa kama Nchi iliyohamwa, yaani Nchi ambayo wakazi wake ama walishakufa siku nyingi kwa homa ya kipindu pindu ama vita hivyo nyumba zao zimebaki kuwa magofu.
Sikuweza kulog in kwa acc yangu kwa kuhofia usalama wangu dhidi ya ‘malaika’.
Maswali mengi yakaibuka kichwani mwangu…
[ol]
[li]Je, Jf itarudi kuwa maarufu kama mwanzo?[/li][li]Je, Max anafanya nini kuwahakikishia watu usalama wao kama mwanzo?[/li][li]Je, mijadala moto moto inaendelea kama ilivyokuwa mwanzo bila kuathiriwa na ‘malaika?’[/li][li]…[/li][li]… Nk. Kwa hakika Jf inatia huruma mno.[/li][/ol]
Imerudi kama boshen tu, ila hapo tambua yafuatayo yanasikitisha option inayokuja utaingia kwa id yako ile ile ila itakuomba kwanza uingize email yako tena na namba yako ya simu hadi utumiwe. Veritification code ndio utafanikiwa kuanza kupost, id itakuwa fake ila email na namba yako ya sim watakuwa nayo, tofauti na wengi wanavyozan eti tutajisalili kwa majina halisi je nikiweka la mtu mwingine watantambuaje?
Hapo watabana tu kwenye namba zenu za simu mziweke kisha mtumiwe veritification code ndio uweze kutumia, ili wakikuhisi wakukamate kilainii… Wait and see jf sio salama tena
Naona ni kama kuna kujisajili upya au kujitambulisha info zako; maana uki - login huwezi post kitu chochote - kuna jambo, ile nyumba bado ya moto wacha tuendelee huku kwanza ugenini. au nyie wenangu vipi??
Kwa hili la kutoa taarifa zako wachangiaji JF watakuwa wachache mno. JF wameibana, unless iwe hosted kwengine, lakini je itajiendeshaje huko? Je anonymous members mtakubali kuichangia ijiendeshe??? Office, Mishahara ya MOD’s, Pango, Server Maintenance etc