Jamii intelligence

Hili jukwaa limedorora sana baada ya kukosa wachangiaji ukilinganisha na la kule jf orijino iliyoko kivuizini.
Sijui ya kuwa wengi wana intellijensia hawajaja huku ukimbizini au wame wamevunjika moyo kwa jambo walilo/tulilo fanyiwa kule home baada ya TCRA kutoa amri ya mitandao hususan jf kusitisha huduma mpaka wajisajili!?

Ngoja niandae nondo nije kuichangamsha.

Bado member wengi hawajajua huku ukimbizini. Lakini taratibu naanza kuona wengi wanaanza kupajua. Kumbuka hakuna tangazo rasmi kwamba kuna mchepuko huku. Ndani muda wa mwezi kutakuwa na member wengi tu. Nikiangalia hata wiki iliyopita majukwaa mengine yalikuwa na post chache na michango haikuzidi page 2. Lakini sasa naona villager kibao humu.

Watakuja tu

Leteni nondo tujichangamshe, kwa kuwa wengi bado hawajaisanukia hii KT.

Labda hawajiamini tena

Nyie nikiwaletea nondo za kiitelejensia si ntabaki nahojiana mwenyewe humu ndani