HURUMA YA MUNGU ISIYO NA KIKOMO!

“MBEGU ZA UZIMA”
Jumapili, April 3, 2016.
Dominika ya Pasaka (Dominika ya 2 ya Pasaka)

Mdo 5: 12-16;
Zab 118: 2-4, 22-27
Ufu 1: 9-13, 17-19;
Yn 20:19-31

HURUMA YA MUNGU ISIYO NA KIKOMO!

"Hakuna mtu atakayetengwa na huruma ya Mungu; kila mtu anajua njia ya kuipata huruma hiyo na Kanisa ni nyumba inayowakaribisha wote na hakuna anayekataliwa. Milango yake inabakia wazi, ili wote wanaoguswa na huruma waweze kupata toshelezo la msamaha. Dhambi inavyokuwa kubwa, vivyo hivyo upendo unapaswa Kuwa mkubwa ule ambao unatolewa na Kanisa kwa wale wote wanaoongoka… Kwa sababu hii, nimeamua kuitisha Jubilei ya hali ya pekee ambayo ni kuwa na huruma ya Mungu katika kiini chake. Unapaswa uwe mwaka mtakatifu wa Huruma. Twahitaji kuuishi mwaka huu katika mwanga wa maneno ya Bwana: “Kuwa na huruma, kama tu Baba yako alivyo na huruma. (Rej. Lk 6:36).” Haya yalikuwa ni maneno ya Papa Francis alipoutangaza mwaka 2016 kuwa ni “Mwaka Mtakatifu wa Huruma.”

Leo katika Dominika ya Huruma ya Mungu, tunakumbushwa juu ya huruma ya Mungu isiyo na kikomo. Injili Leo inaonyesha mamlaka ya Yesu pale anapowapa mitume, Roho Mtakatifu, ambaye atakayetoa msamaha wa dhambi.

“Mungu hachoki kamwe kutusamehe; sisi ndiyo tunaochoka kuitafuta huruma yake. Yesu Kristo, aliyetuagiza tusameheane “saba mara sabini” (Mt 18:22) ametupa mfano wake yeye mwenyewe: ametusamehe saba mara sabini… kwa upole usiyotuacha tuaibike, lakini daima wenye uwezo wa kuturudishia furaha yetu, anatuwezesha kuinua vichwa vyetu na kuanza upya. Basi sisi tusiukimbie ufufuko wa Yesu, kamwe tusikate tamaa, hata litokee jambo gani. Maisha yake yawe mfano unaoangazia zaidi ya kitu chochote, unaotusukuma kwenda mbele!” (Furaha ya Injili, 3)

Sala: Bwana, Nisaidie kamwe nisiwe mbali nawe, badala yake niiamini huruma yako. Amina.

DOMINIKA YA PILI YA PASAKA (DOMINIKA YA HURUMA YA MUNGU)

SOMO 1
Mdo 5:12-16

Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani; na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha; walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake; hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao. Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab 118:2-4, 13-15, 22-24

(K)Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
Mlango wa Haruni na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
Wamchao Bwana na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele. (K)

Ulinisukuma sana ili nianguke;
Lakini Bwana akanisaidia.
Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu,
Naye amekuwa wokovu wangu.
Sauti ya furaha na wokovu
Imo hemani mwao wenye haki. (K)

Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu.
Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana,
Tutashangilia na kuifurahia. (K)

SOMO 2
Ufu 1:9-11a, 12-13, 17-19

Mimi Yohane, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa sabaNikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini. Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

INJILI
Yn 20:19-31

Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa. Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Good read. Next time, shorter would be perfect.

Purr!! If you must spread the word, Pris use a engrich

@Female Perspective you also beleive am purr?

tumsifu yesu christo?..

Enda ukamuliwe na priest.